Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Buruhani Nyenzi (kushoto) akimkabidhi cheti za pongezi Mshindi wa Tuzo ya mwanahabari Bora mitandao ya kijamii (Online Media) wa habari za Hali ya Hewa Tanzania katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika leo Oktoba 30, 2023 Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Buruhani Nyenzi (kushoto) akimkabidhi cheti za pongezi Bw. Mussa Khalid mshindi wa jumla katika kipengele cha Runinga na Radio katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika leo Oktoba 30, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Buruhani Nyenzi (kushoto) akimkabidhi cheti za pongezi mshindi wa Tuzo ya habari za Hali ya Hewa kutoka Gazeti la Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Bi. Pamela Chilongola katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Oktoba 30, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu wa Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC);
Dkt. Ladislaus Chang’a akifafanua jambo katika hafla ya utoaji tuzo ya wanahabari Bora wa habari za Hali ya Hewa iliyofanyika leo Oktoba 30, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Washindi wa Tuzo ya wanahabari Bora wa habari za hali ya hewa mwaka 2023 wakiwa katika picha ya pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Buruhani Nyenzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu wa Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC); Dkt. Ladislaus Chang’a.
……..
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo Oktoba 30, 2023 imewatangaza washindi wa Tuzo ya wanahabari Bora wa Taarifa za Hali ya Hewa Tanzania kwa mwaka 2023.
Washindi wa Tuzo hizo Mwandishi wa habari Bw. Noel Rukanuga ambaye ameshinda Tuzo ya Mwanahabari Bora wa mitandao ya kijamii (Online Media) wa habari za hali ya Hewa Tanzania, Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Bi. Pamela Chilongola, huku Mussa Khalid akibuka mshindi wa jumla katika kipengele cha Runinga na Radio.
Akizungumza leo Oktoba 30, 2023 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya utoaji tuzo ya mwanahabari bora wa taarifa za hali ya hewa, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Buruhani Nyenzi, amesema kuwa wanahabari wanafanya kazi kubwa katika kuelimisha jamii, hivyo utoaji wa Tuzo hizo ni ishara ya kutambua mchango na kuthamini kazi za waandishi wa habari katika utoaji wa taarifa za hali ya hewa kwa jamii.
Dkt. Nyenzi amesema kuwa ni mwaka wa nne mfululizo kwa tuzo hizo kutolewa na TMA kwa lengo la kutambua baadhi ya kazi za wanahabari ambazo zimekuwa na matokeo bora zaidi katika kuhabarisha na kuelimisha umma.
“Mchango wenu ni mkubwa kwa kuwezesha jamii kutumia taarifa za Hali ya Hewa katika kujilinda na kupunguza athari mbaya za hali ya hewa sambamba na kuijengea jamii uwezo wa kutumia taarifa za hali ya hewa kwa maendeleo yao ya kiuchumi” amesema Dkt. Nyenzi.
Amesema kuwa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa inaipongeza Kamati iliyohusika katika kuchambua taarifa zilizowasiilishwa kwa kuzingatia vigezo vilivyokubalika na kuwapata washindi wa tuzo.
“Kwa niaba ya Bodi na Menejimenti ni furaha kubwa kwangu kuwatunuku washindi wa tuzo hii kwa mwaka huu 2023, niwatakie ushiriki mwema wanahabari wote katika mwaka ujao” amesema Dkt. Nyenzi.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu wa Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC);
Dkt. Ladislaus Chang’a, amewapongeza washindi pomoja na wahababari wote kwa kuendelea kuripoti taarifa za hali ya hewa kwa jamii.
Amewakumbusha wanahabari kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa TMA kuelezea na kusisitiza umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwa jamii katika shughuli zao za kila siku.
Meneja Mahusiano wa TMA Bi. Monica Mutoni, amesema kuwa washindi wote wamefanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuwasilisha taarifa yenye ubunifu.