Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa (Mb) amewaongoza Mawaziri, Wabunge, Watumishi wa Ofisi ya Bunge, Viongozi na Wananchi Mbalimbali katika mapokezi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) leo tarehe 31 Oktoba, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Jijini Dodoma. Mheshimiwa Dkt. Tulia amewasili nchini baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika Mkutano wa 147 wa Umoja huo uliofanyika Jijini Luanda, Angola.