……..,……….
NJOMBE,Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imesema inapokea maombi 10 hadi 15 kwa mwezi ya wazazi kupima vinasaba(DNA)kwa ajili ya mahusino ya baba na watoto.
Akieleza mapokeo ya wananchi katika monesho ya Sido yanayofanyika kitaifa mkoani Njombe katika viwanja vya Sabasaba Fundi sanifu mwandamizi Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Rashidi Mjema amesema uhitaji wa kupima vinasaba DNA ni mkubwa kutokana na udanganyifu ambao unatokea kwa wale labda wanawabambikia wababa watoto ambao sio wa kwao.
‘’Lakini hii pia ni kwa wababa ambao pia wanakataa majukumu yao pia ni wengi kwa hiyo uhitaji huu ni mkubwa sana kwa sasa hivi’’alisema Mjema.
Aidha Mjema amesema huduma hiyo si ya kumtambua baba wa mtoto tu bali ni teknolojia mbayo pia inabaini wahalifu katika matukio mbalimbali ikiwemo ujambazi.
’’Taratibu ni rahisi tu mteja atatakiwa apitie ustawi wa jamii au kwa mwanasheria anayetambulika au kwa mahakama akishakuja na barua basi tutamtengenezea namba ya malipo ambayo ni sh.300,000 kwa baba,mama na mtoto tutachukua kipimo alafu atasubiri takribani siku 21 hadi 30 za kazi tutampatia majibu yake huo ndio utaratibu mwepesi ambao tunautumia kwa wale ambao wanachangamoto ya kujua uhalali wa baba wa mtoto’’amesema Mjema.
Kwa upande wake mkemia daraja la pili kutoka Wakala ya Mabaara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Ruben Sengelema amezungumzia madhara ya sumu kuvu kwamba ni aina ya sumu inayopatikana kutoka kwa jamii aina ya fangasi ambao wao wanaathiri sana mazao kama vile nafaka zikiwemo mahindi,mchele na karanga.
‘’Sumu kuvu inaweza ikaathiri mazao kwa njia tofauti tofauti iiweo njia moja wapo ni pale ambapo mkulima wa mazao hakufuata taratibu zile zinazotakiwa mpaka kufikisha mazao katika hali ambayo ni ya uhifadhi kwa mfano kiasi ya unyevunyevu kisipozingatiwa katika mazao ‘’alisema Sengelema.
Nao Baadhi ya wananchi waliyoshiriki katika maonyesho hayo yaliyofunguliwa na naibu waziri wa viwanda na biashara na Kish kufungwa makamu wa Rais Dr Philip Isdory Mpango octoba 27 akiwemo Magreth Sanga wameishukuru serikali kwa kuleta huduma hiyo katika monesho kwasababu watu watu wajaijua kwani miaka ya karibuni wanaume wengi wanakimbia majukumu Yao kwa kisingizio Cha kubambikizwa watoto.
“Niwashauri akina mama na akina baba kwenda kwenye Banda la maabara ya mkemia mkuu wa serikali ili kujua taratibu za DNA ili wapime na kuwanasa akina baba wanaowapa ujauzito Wanawake na Kisha kuwakimbia kwa madai ya kwamba sio wao”amesema Sanga.
Licha ya kufungwa octoba 27 lakini serikali ya mkoa wa Njombe umeongeza siku nne mbele ili kutoa fursa zaidi kwa wajasiriamali kutangaza bidhaa na mtandao mpya wa biashara.