Na Mwandishi wetu, Iringa.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoani Iringa, *Dkt Tumaini Msowoya* amelaani matukio ya kikatili dhidi ya watoto likiwemo la baba kumnyonga mwanae huku akijirekodi video.
Juzi, vyombo vya habari vimetoa taarifa ya baba kutoka eneo la Mlandege Manispaa ya Iringa ambaye alimuua mwanae kwa kumnyonga huku akijirekodi.
Dkt Msowoya alikuwa akizungumza na mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki, Kigango cha Mbigili wakati alipo muwakilisha Mbunge wa Jimbo la Kilolo, *Mh Justine Nyamoga* kwenye uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Mt Augustino.
“Ni vizuri kuzungumza na kukemea matukio haya ya ukatili yanayo utia doa mkoa wetu, viongozi wa dini wala msikae kimya kemeeni,” amesema na kuongeza;
“Hii ni hatari, wakati Rais Samia Hassan Suluhu anapambana kuboresha miundo mbinu ya elimu, watoto wanafanyiwa ukatili bila hutuma. Sasa tuseme basi,”
Kwaya ya Mt Augustino wamefanikiwa kuzindua albamu yao ya kwanza *Enyi watu wa Mataifa* ikiwa na nyimbo nane.
Viongozi mbalimbali akiwemo Diwani wa Kata ya Lugalo na Nyalumbu walihudhulia uzinduzi huo ambao ulikusanya zaidi ya kwaya 10 kutoka madhehebu mbalimbali.