Maadhimisho ya siku ya Lishe kitaifa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe yamefanyika leo katika uwanja wa shule ya Msingi Katumba II , Mgeni Rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu.
Mhe Haniu amepongeza kwa hatua nzuri ya lishe iliyofikiwa katika Wilaya ya Rungwe akitaja kuwa Udumavu kwa watoto kwa sasa umefikia asilimia 26%
Mhe Haniu ameeleza kuwa Takwimu hizi zimewezekana baada ya wananchi kuanza kuitikia wito wa kula chakula bora chenye viini lishe na hivyo kuondoa Utapiamlo Pamoja na Udumavu.
Ameeleza kuwa changamoto ya ukosefu wa lishe itazidi kutokomezwa kwa kuendelea kutoa elimu ya uelewa wa masuala ya lishe katika jamii, ngazi ya familia, watendaji na viongozi wa serikali.
Aidha lishe imesaidia kupandisha kiwango cha ufaulu ambapo katika mitihani ya utamilifu(MOCK) pamoja na Taifa(NECTA) wanafunzi wamekuwa wakifanya vizuri kutokana na lishe.
Kwa miaka mitano mfululizo Rungwe imekuwa ikishika nafasi ya pili katika Mkoa wa Mbeya baada ya Jiji katika mitihani yote na mpango ni kushika nafasi ya kwanza 2023/2024
Mpaka sasa wanafunzi wanapata chakula cha mchana kwa asilimia 100% katika shule za msingi na Sekondari.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya haya ni “Lishe bora kwa vijana Balehe, Chache ya Mafanikio yao”
Kauli hii imepewa kipaumbele kwa Vijana kuelimishwa kuwa lishe bora husaidia kujenga mwili, kulinda mwili pia husaidia kumuandaa kijana kuwa mzazi bora kwa kuimarisha mifumo ya uzazi.
Naye afisa Lishe Wilaya ya Rungwe Bi.Halima Kametha ameongeza kuwa Lishe bora hutunza mwili wa kijana na kumfanya achelewe kuzeeka, hivyo kuongeza muda wa kufanya kazi(Productivity time) na kuongeza pato la taifa kwa kupunguza wategemezi ( Dependence Population)