NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DAR ES SALAAM
WAJUMBE
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, wameridhishwa na
huduma zitolewazo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) baada ya kusikilzia
ushuhuda wa baadhi ya wanufaika wa fidia wakati wa ziara ya Kamati ya kutembelea
ofisi za Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 28, 2023.
Wajumbe
hao walioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Riziki Lulida, walipata
fursa ya kupata maelezo ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko kutoka kwa watendaji
wa Mfuko, kabla ya kusikiliza ushuhuda
“Niwapongeze
WCF kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya, nitapeleka salamu kwa Mhe. Rais ambaye
amekuwa mstari wa mbele kusaidia makundi mbalimbali yakiwemo ya wanawake, Vijana na wenye ulemavu,na hili mnalofanya mnamfanya ajivunie huduma mnazotoa kwa wananchi.”
Alisema Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Riziki Lulida.
Naye
Mhe. Katani Ahmed Katani, yeye ameshauri Mfuko ujielekeze sana kwenye utoaji wa
elimu, ili uwanufaishe watu wengi zaidi.
“Kwa
saabu mnaenda vizuri ni matarajio yetu wanaopata ajali kazini ninyi ndio
mtakaowafuta machozi
Bi.
Ester John, yeye ni mnufaika wa fidia kama mtegemezi, mumewe ambaye alikuwa
mtumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, alifariki katika ajali
ya gari wakati akitekeleza majukumu ya mwajiri wake.
“Wakati
tunampoteza mpendwa wetu, mimi nilikuwa ugenini, sina ndugu yoyote nilifanyiwa
operesheni ya uzazi, WCF, ilitusaidia, Mafao ya kila mwezi ninayoyapokea yanasaidia
kuendesha maisha yangu mimi pamoja na mtoto.” Alisema.
Mnufaika
mwingine, Bw. Hassan Jambau, yeye aliwaambia wajumbe hao kuwa tangu alipoumia
hadi kupona na kubaki mlemavu wa mguu, WCF imekuwa pamoja naye.
“Sina
mengi ya kusema, zaidi ya kutoa shukrani nyingi kwa WCF.” Alisema.
Kwa
upande wake, Bw. Kelvin Mwemezi, ambaye naye aliumia mguu baada ya kuchomwa na
kitu chenye ncha kali, alisema, Mfuko umekuwa msaada mkubwa na umekuwa kama
sehemu ya familia yake baada yay eye mwenyewe kupoteza wazazi wake.
“Namshukuru
sana Mheshumiwa Rais, kwa kuanzisha Mfuko huu, nawashukuru sana ninyi viongozi
na wafanyakazi wa WCF, nilikuwa nimekata tama ya maisha baada ya kuumia, na
mama yangu kufariki, lakini Mfuko umenifuta machozi.” Alisema.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemabvu), Mhe. Patrobas Katambi, aliwashukuru wajumbe wa Kamati hiyo kwa
kutembelea WCF ambao iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
“Napenda
kumshukuru sana Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye yeye ndiye ametuwezesha kwa
kutupatia vitendea kazi ambavyo vinatusaidia kutekelza majukumu ya kulipa fidia
kama mlivyopata ushuhuda hapa.” Alisema.
Aidaha,
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhandisi,
Cyprian Luhemeja, aliutaka Mfuko uendelee na kampeni ya kutoa elimu na iwe
kampeni endelevu, ili umma wa watanzania wengi wajue huduma nzuri zinazotolewa
na Mfuko.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma amesema, WCF imeendelea
kujenga mifumo ya kufanyia kazi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa
wanachama.
“Zaidi
ya asilimia 90 ya huduma zinapatikana kwa njia ya mtandao.” Alifafanua.
Lulida (katikati), akisalimiana na mnufaika wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Hassan Jambau, mara baada ya kutoa ushuhuda wake mbele ya wajumbe wa Kamati Oktoba 28, 2023. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi.
na Wenye Ulemavu, Mhandisi, Cyprian Luhemeja, akifafanua jambo wakati akizungumza na wajumbe hao.
Lulida (wapili kushoto) akizungumza mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi, (watatu kushoto), Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian Luhemeja (wakwanza kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini WCF, Bw. Emmanuel Humba (wanne kushoto) na Bi. Rifai Mkumba, Makamu Mwnyekiti WCF.