Na Ashrack Miraji
(Same) kilimanjaro
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amezindua jengo la Mama na mtoto katika kituo cha afya Bwambo Wilayani Same kinacho milikiwa na kanisa katoliki jengo lililogharimu kiasi cha shilingi Milioni 450.
Akizungumza mara banda ya kuzindua jengo hilo ambalo limejegwa kwa ufadhili wa Shirika la partner for Hope lililopo Nchini Marekani Mkuu huyo wa Mkoa ameshukuru kanisa katoriki kushirikiana na serikali katika kusogeza huduma kwa wananchi.
“Kuwa na jengo hili la Mama na mtoto imekuwa msaada mkubwa kwa jamii hasa akina mama wanao jifungua watoto njiti, sisi kama Serikali hatuna budi kuwashukuru kwa kuokoa maisha ya Mama na mtoto pia nawaomba wananchi wanufaika kuendelea kutumia huduma hii kwani ni sehemu ya uimalishaji wa huduma za afya kati ya kanisa na Serikali”.amesema Nurdin Babu.
Kwa upande wake Askofu wa jimbo la Same Mkoani Kilimanjaro Mhashamu Rogath Kimario ametoa shukrani kwa Serikali kwa ushirikiano kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha huduma muhimu, akishukuru pia viongozi wa kanisa kwa usimamizi mzuri kufanikisha Ujenzi wa jengo hilo ambalo limekua msaada kwa wakazi wa Same wakiwemo waumini wa kanisa hilo kuwa na uhakika wa matibabu na huduma nyingine za kiafya.
Nae Mkuu wa wilaya ya Same Kaslida Mgeni amesema kupatikana kwa mradi huo ni matokeo ya kuimarika kwa ushirikiano baina ya serikali na tasisi mbalimbali zikiwemo za binafsi kutambua umuhimu wa kushiriki kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii.
“Walicho kifanya wenzetu wa kanisa katoliki ni Jambo la kushukuru na hii sio Mara ya kwanza kwani tumekua na ushirikiano mzuri sisi kama serikali na wenzetu wa mashirika binasfi hakika wamefanya kazi kubwa pokeeni salamu za shukrani kwa niaba ya wakazi wa wilaya ya Same”.Alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya same.
“Kama serikali pia tunaendelea kutoa rai kwa taasisi nyingine za dini na ambazo siyo za dini kuunga mkono juhudi za serikali chini ya Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kuleta maendeleo chanya kwenye wilaya ya Same na Taifa kwa ujumla”.Amesema Mkuu huyo ya wilaya.