Katibu Tawala Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Hassan Mkwawa akizungumza na wananchi na wadau kutoka taasisi mbalimbali ambao wamejitokeza kufanya usafi wa Mazingira wa mwisho wa Mwezi leo katika kata ya Makuburi kwenye Wilaya hiyo.
Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Elisony Mweladzi akizungumzia dhamira Yao ya kufanya usafi Mazingira wa mwisho wa Mwezi leo katika kata ya Makuburi Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam.
Diwani wa Kata ya Makuburi Olivery Shirima akizungumza na wananchi na wadau kutoka taasisi mbalimbali ambao wamejitokeza kufanya usafi wa Mazingira wa mwisho wa Mwezi Leo katika kata ya Makuburi kwenye Wilaya hiyo.
Baadhi ya wadau mbalimbali ambao wameshiriki katika zoezi la ufanyaji wa usafi wa mwisho wa mwezi Leo katika kata ya Makuburi Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam wakiwa Kwenye picha ya Pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo.
……..,…………….
NA MUSSA KHALID
Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam imeendelea kuwasisitiza wananchi wa Wilaya hiyo kufanya usafi katika maeneo yao ikiwemo kuepuka kufanyabiashara pembezoni mwa barabara ili kuweka Mazingira katika Hali ya Usafi.
Kauli hiyo imetolewa Leo jijini Dar es salaam na Katibu Tawala Wilaya ya Ubungo Hassan Mkwawa wakati akizungumza na wananchi na wadau kutoka taasisi mbalimbali ambao wamejitokeza kufanya usafi wa Mazingira wa mwisho wa Mwezi katika kata ya Makuburi kwenye Wilaya hiyo.
Amesema walianzisha kampeni ya kataa uchafu,safisha,Pendezesha Ubungo Ili kuwakumbusha watu kuwa shughuli za usafi ni endelevu na kuwajengea watu tabiaa ya kuona usafi ni ya Kila siku.
Aidha Katibu Tawala Huyo ametumia fursa hiyo kuwasisitiza TANROADS kusimamia vyema maeneo ya hifadhi ya barabara kwa kuangalia namna Bora ya kuyapangilia vyema ikiwemo kupanda Miti au maua ili kuepusha watu kujitokeza kufanya biashara katika maeneo hayo.
“Tumeamua pia kutoa zawadi Kwenye Kampeni hii kama motisha ya mitaa ambayo itafanya vizuri ambapo mtaa wa kwanza utakaofanya vizuri utapewa pikipiki Mbili ambapo moja itakuwa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi Mwenyekiti wa Mtaa na Nyingine kwa ajili ya ofisi Mtendaji wa Kata husika na mtaa wa mwisho upawekewa bendera ya picha ya uchafu na takataka itapepereshwa mpaka pale utakapozingatia usafi”amesema Katibu Tawala Ubungo
Akishiriki Kwenye zoezi Hilo la usafi wa mwisho wa mwezi,Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Elisony Mweladzi ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wananchi kuzitunza barabara kwa kutotupa takataka hovyo kwenye mitaro iliyopo pembezoni mwa barabara kwani ni adui Mkubwa wa rasilimali za barabara.
Pia Mhandisi Mweladzi amewasihi wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam hususani wa Wilaya ya Ubungo kutofanya Biashara zao kwenye hifadhi ya barabara kwani ni hatarishi wanaweza kupata ajali lakini ni uchafuzi hivyo amewataka kuacha hifadhi hizo kutumika kwa malengo mahususi.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Makuburi Olivery Shirima amesema atahakikisha analisimamia vyema suala la usafi kwenye kata ikiwa ni sambamba na kupanda miti ili kuipendezesha na kuwa ya mfano katika Wilaya hiyo.
Naye Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Kibangu Kata ya Makuburi Desideri Ishengoma amesema kumekuwa na muitikio mkubwa katika zoezi hilo na kuwasisitiza wananchi kuendelea kuunga mkono suala la usafi na sio kuona kama ni la Viongozi pekee bali ni la watu wote.
Baadhi ya wadau wakiwemo wa Michezo ya jogging na mabondia ambao wameshiriki kwenye zoezi hilo la usafi wa mwisho wa mwezi Kwenye kata hiyo wamesema wataendelwa kuwahamasisha wananchi kuwa mabalozi bora wa kuipendezesha Ubungo Ili iendelee kuwa katika Hali ya Usafi.
Zoezi Hilo la usafi wa mwisho wa mwezi ambalo limefanyika Leo Kwenye Kata ya Makuburi Wilaya ya Ubungo likiongozwa na Afisa Mazingira anayeshughulikia Udhibiti wa takangumu na Usafirishaji Manispaa ya Ubungo Lawi Bernad limewashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa vyama,wanamichezo, TANROADS,kwa Pamoja wakiitikia wito wa kampeni ya kataa uchafu,safisha,Pendezesha Ubungo ambayo ilizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo hivi karibuni.