Na Mwandishi Wetu, Tanga.
Wakazi wa Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga wameishukuru Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kuwasaidia kiuchumi na kufanikiwa kuishi katika mazingira rafiki tofauti na awali.
Hatua hiyo imekuja baada ya serikali kupitia TASAF kwa mwaka huu 2023 kutoa zaidi ya Shilingi bilioni nne katika Wilaya ya Mkinga kwa ajili ya kusaidia kaya maskini.
Mkazi wa Kijiji Cha Bamba Malongo Wilaya ya Mkinga Bi. Halima Mfalme, amesema kuwa wanafuraha kubwa baada ya kunufaika katika mpango wa TASAF.
Amesema kuwa baada ya kunufaika na mradi wa TASAF kwa sasa wanakula chakula milo miwili tofauti na awali kwani walikuwa wanakula mara moja kwa siku.
Nae Sharobati Nyiwa amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassani kwa kuendelea kuwasaidia kupitia mradi wa TASAF.
“Nashukuru kwa sasa maisha yamekuwa mazuri, familia yangu inakwenda shule kupitia mradi wa wangu ambao nimewezeshwa na TASAF” amesema Nyiwa.
Amesema kuwa amefanikiwa kufungua biashara ya kuuza dagaa ambayo imekuwa na faida na kuleta tija katika maendeleo ya maisha yao.