Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila akifunga rasmi Mkutano Mkuu wa Waandishi wa Habari mkoa wa Dar es Salaam, tarehe 27 Oktoba, 2023, Dar es Salaam.
Bi. Joyce Makwata, mchambuzi wa Hali ya Hewa TMA, akiwasilisha mada wakati wa Mkutano Mkuu wa Waandishi wa Habari mkoa wa Dar es Salaam, tarehe 27 Oktoba, 2023, Dar es Salaam.
Bi. Monica Mutoni, Msimamizi Kitengo cha Masoko na Uhusiano, TMA, akiwasilisha akijibu maswali wakati wa Mkutano Mkuu wa Waandishi wa Habari mkoa wa Dar es Salaam, tarehe 27 Oktoba, 2023, Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa wakati wa Mkutano Mkuu wa Waandishi wa Habari mkoa wa Dar es Salaam, tarehe 27 Oktoba, 2023, Dar es Salaam.
……………………..
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa elimu kwa waandishi wa habari mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kuhusu sayansi ya hali ya hewa ikiwemo suala la ElNino na huduma zitolewazo na Mamlaka, katika Mkutano Mkuu wa waandishi hao unaofanyika Dar es Salaam, tarehe 27 hadi 28 Oktoba, 2023.
Katika Mkutano huo uliofuguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, TMA iliwasilisha mada na kutoa fursa kwa waandishi wa habari kuuliza maswali pamoja na kutoa maoni mbalimbali ya uboreshaji na usambazaji wa huduma za hali ya hewa nchini.