Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Asha Juma Khamis akipokea vifaa kwaajili ya kuboresha utendaji kazi wa idara hiyo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji Benki ya watu wa Zanzibar PBZ DK Muhusini Salum Masoud Mpirani Mjini Unguja.
…….
Benki ya watu wa Zanzibar imekabidhi vifaa mbali mbali kwa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar ili kuboresha utendaji kazi wa idara hiyo.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mkurugenzi mtendaji PBZ Dk.Muhsin Salim Masoud alisema vifaa hivyo vitaondoa upungufu wa vitendea kazi katika Ofisi hiyo.
Hata hivyo amesema PBZ itakua mbele muda wowote kuuunga mkono jitihada za Idara hiyo katika kuhakikisha inaendelea kufikisha taarifa za utendaji wa Serikali kwa jamii.
Aidha amesema PBZ imetoa vifaa hivyo ikiwa ni mwendelezo wao wa kujenga mahusiano mema na taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi ili kuona zinatekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Sambamba na hayo alisema kuelekea maadhimsho ya miaka 60 ya Mapinduzi Benki hiyo inatarajia kuzindua miradi mbalimbali inayolenga kuboresha huduma za benki kwa jamii.
Akifafanua baadhi ya miradi hiyo alisema ni pamoja na ufunguzi wa Tawi la Malindi, Forodhani, Mlandege, Amani Nungwi, Morogoro, Mbeya, Michenzani pamoja na uzinduzi wa mfumo mpya wa Mobile na internet benki.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Asha Juma Khamis alisema vifaa hivyo ni njia moja wapo itakayopelekea wafanya kazi kutekeleza majukumu yao ya kufikisha taarifa kwa jamii kwa wakati.
Pia ameishukuru PBZ kwa kushirikiana na Taasisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini PDB katika kufanikisha upatikanaji wa vifaa hivyo vinavyoenda kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji katika Idara hiyo,na kuahidi kuvitunza na kuvifanyia kazi zilizokusudiwa.
Naye Mkuu wa habari na Mawasiliano kutoka (PDB) Mohamed Manssor aliwataka Maafisa wa Idara ya Habarai maelezo kuhakikisha wanavifanyia kazi iliyokusudiwa ili kufikia malengo ya Serikali katika Idara hiyo.
Katika makabidhiano hayo Idara ya habari Maelezo ilipokea vifaa mbali mbali vya kiutendaji ikiwemo Laptop na Scaner.
Picha no 8582, 8580 na 8583:Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Asha Juma Khamis akipokea vifaa kwaajili ya kuboresha utendaji kazi wa idara hiyo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji Benki ya watu wa Zanzibar PBZ DK Muhusini Salum Masoud Mpirani Mjini Unguja.
Picha no 8570 na 8574:-Mkurugenzi Mtendaji Benki ya watu wa Zanzibar DK. Muhusini Salum Masoud akizungumza na maafisa wa Idara ya Habari Maelezo wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi vilivyotolewa na PBZ ili kuboresha utandaji kazi wa idara hiyo.
Picha no 8565:-Mkuu wa habari na Mawasiliano Mohamed Mansour kutoka Taasisi ya Afisi ya Rais,Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini(PDB) akizungumza na wakuu wa PBZ na Maafisa Habari kutoka Habari Maelezo baada ya makabidhiano ya vitendea kazi vilivyotolewa na PBZ ili kuboresha utandaji kazi wa idara hiyo.
Picha na Fauzia Mussa HABARI MAELEZO ZANZIBAR.