Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Bw. Titus Kaguo akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 10, 2023 Jijini Dar es Salaam
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imevifungia vituo viwili vya mafuta kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kuhodhi mafuta ili kujipatia maslahi haramu ya biashara ikiwemo faida kubwa kutokaba na ongezeko la bei za mafuta jambo ambalo ni kinyume na sheria, kanuni na miongozo inayosimamia biashara ya mafuta nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27, 2023 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA Bw. Titus Kaguo, amesema kuwa vituo vilivyofungiwa ni Kituo cha GAPCO Tanzania Limited Moshi Service Station chenye namba ya leseni PRL – 2023 – 104 kilichopo Moshi Kilimanjaro.
Bw. Kaguo amesema Kituo kingene ni Anwar Saleh Bakhamis T/A Serious Oil Petrol Station yenye usajili wa leseni PRL – 2019 -228.
Amesema kuwa vituo hivyo wamefanya kasa la kufunga vituo vya kuuza mafuta wakiwa bado wanamafuta jambo ambalo ni wamekiuka masharti ya uuza wa mafuta.
Bw. Kaguo amesema kuwa mpaka sasa jumla wamevifungia vituo vya kuuza mafuta 11 kwa kosa la kwa kosa la kuhodhi mafuta ili kujipatia maslahi haramu ya biashara ikiwemo faida kubwa kutokaba na ongezeko la bei za mafuta jambo ambalo ni kinyume na sheria, kanuni na miongozo inayosimamia biashara ya mafuta nchini.
“EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara ya mafuta nchini kuhakikisha wanaendesha biashara zao kwa mujibu wa sheria, kanuni, na miongozo inayosimamia biashara ya mafuta nchini” amesema Bw. Kaguo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Petroli, sura Na 392 EWURA ina jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa mafuta wakati wote katika maeneo yote nchini.
Kuanzia mwezi Julai mwaka huu kumekuwepo na matukio kwa baadhi ya maeneo hasa pembezoni mwa nchi kukosa mafuta hasa kipindi bei zinapoelekea kubadilishwa na kusababisha kuwa na usumbufu makubwa kwa wananchi na madhara ya Kiuchumi.
Ili kufikia malengo EWURA inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kisheria ikiwemo kuvifungia baadhi ya vituo vilivyothibitika kufichua mafuta kinyume na kanuni na miongozo inayosimamia biashara ya mafuta nchini.