Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Fredrick Mtui (wa pili kulia) akimkabidhi funguo mshindi wa pikipiki Anne Chimenya ( wa pili kushoto) baada ya kushinda droo ya pakua app ya Y9 Microfinance. Wa kwanza kulia ni Meneja Masoko wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Sophia Mang’enya ambapo wa kwanza kulia ni mshindi wa simu wa droo hiyo, Jacqueline Jumla na katikati ni Afisa Msimamizi wa michezo ya bodi ya kubahatisha nchini, Elibariki Sengasenga .
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Fredrick Mtui (kulia) akimkabidhi simu mshindi wa droo ya pakua app ya Y9 Microfinance Jacqueline Jumla.
Meneja Masoko wa Taasisi ya Y9 Microfinance, Sophia Mang’enya (katikati) akizungumza wakati wa droo ya tatu ya pakua app ya Y9 na kupata huduma ya tatu za kupata mkopo ikiwa fedha taslimu, mkopo wa fedha ya kununua umeme na muda wa maongezi. Kulia ni Afisa Msimamizi wa michezo ya bodi ya kubahatisha nchini, Elibariki Sengasenga na kushoto ni mshindi wa simu wa droo ya pili, Jacqueline Jumla.
….
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance imekabidhi Anne Chimenya zawadi yake ya pikipiki baada ya kuibuka mshindi katika droo ya pili ya kampeni ya pakua app ya Y9 Microfinance na kupata huduma ya tatu ambazo ni mkopo wa fedha taslimu, mkopo wa fedha ya kununua umeme na mkopo wa fedha ya kununua muda wa mongezi.
Anne alikabidhiwa zawadi hiyo na Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Fredrick Mtui ambaye pia aliwaomba Watanzania kuendelea kupata huduma zao kuingia katika droo.
Mtui alimpongeza mshindi huyo kwa kujiunga na huduma zao na kuweza kushinda. Mbali ya Chimenya, Mtui pia alikabidhi mshindi wa simu ya mkononi, Jacqueline Jumla ambaye ni mkazi wa Ubungo External.
Alisema kuwa washindi hao wameshinda zawadi hizo baada ya kukopa kupitia app yao na baada ya kutumia mikopo hiyo, walirejesha ndani ya siku tatu kwa mujibu wa taratibu.
Alisema kuwa zawadi bado zipo nyingi na kuwaomba Watanzania kuendea kutumia huduma zao. “ Tutakuwa na droo ya kila wiki na kuwazawadia washindi wawili. Mshindi wa pikipiki na simu janja ya mkononi. Hii ni fursa kwa wateja wetu,” alisema Mtui.
Kwa upande wake, Anne alisema kuwa alikopa Sh4,000 tu kwa ajili ya matumizi yake na mbali ya kuweza kutatua tatizo lake, bado amefaidika kwa kushinda pikipiki.
“Nimefurahi sana, nilikopa Sh4,000 tu, huwezi kuamini, mbali ya kutatua matatizo yangu, nimeweza kushinda pikipiki. Naowamba watanzania kutumia fursa kwa kupakua app ya Y9 microfinance na kushinda,” alisema Anne.
Kwa upande wake, Jacqueline Jumla alisema kuwa amefarijika sana na zawadi hiyo ya simu na kuahidi kuendelea kutumia app ya kampuni hiyo.
Wakati huo huo, taasisi hiyo imewapata washindi wa droo wengine wa droo ya pakua app ya Y9 ili uweze kupata huduma tatu za mikopo.
Washindi hao ni Eva Mbena mkazi wa Ruvuma aliyeshinda pikipiki na Godfrey Chuma ambaye pia ni mkazi wa Ruvuma ambaye ameshinda simu ya mkononi.
Washindi hao watazawadiwa zawadi zao katika droo ya wiki ijayo kwa mujibu wa Meneja Masoko wa Taasisi ya Y9 Microfinance, Sophia Mang’enya.
Mang’enya alisema kuwa taasisi yao itaendelea kuwawezesha Watanzania kwa kupitia droo hiyo ambapo katika droo ya mwisho, mshindi ataibuka na zawadi ya gari aina ya Toyota IST.
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa michezo ya bodi ya kubahatisha nchini, Elibariki Sengasenga aliipongeza washindi hao na kuwaomba Watanzania kutumia fursa hiyo ili kufikia malengo yao.