Mkaguzi wa Hazina Saccos Wizara ya Fedha Bi. Avemaria Lukanga akizungumza katika Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano na Masoko wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha Mkoani Morogoro Oktoba 25,2023.
………………………
NA JOHN BUKUKU, MOROGORO
Taasisi ya Fedha Hazina Saccos imewataka watumishi wa umma kuchangamkia fursa ya kujiunga na Saccos hiyo ili waweze kutatua changamoto mbalimbali zinazotokana na ukosefu wa fedha pamoja na kuongeza utulivu, ufanisi katika utendaji kazi.
Hatua hiyo imekuja baada Hazina Saccos kuna na bidhaa mpya ya mkopo wa “Tuliza Moyo” ambao umelenga kuwa mkombozi wa wafanyakazi wa serikali kupata mkopo na kuachana na mikopo ya kausha damu ambayo imekuwa ikiumiza watu wengi katika jamii.
Akizungumza katika Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano na Masoko wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha Mkoani Morogoro, Mkaguzi wa Hazina Saccos Wizara ya Fedha Bi. Avemaria Lukanga, amesema kuwa baada ya miezi mitatu mwanachama mpya kujiunga anapata fursa ya kukopa mkopo wa dharula shilingi milioni tano na kurudisha ndani ya mwaka mmoja.
Bi. Lukanga amesema kuwa pia kuna mkopo wa elimu shilingi milioni tano ambao unarudisha katika kipindi cha miaka miwili ikiwa na liba ya asilimia 0.84.
Amesema kuwa mfanyakazi wa serikali mwanachama anaweza kukopa shilingi milioni moja na kurejesha katika kipindi cha mwezi moja bila riba.
“Kupitia mkopo huu watu wengi wanatulia makazini na kufanya kazi kwa utulivu bila kuwa na mawazo pamoja na kuheshimika mtaani kutokana ni wanachama wa Hazina Saccos” amesema Bi. Lukanga.
Amesema pia kuna mkopo wa biashara, ujenzi na maendeleo ambapo mkopaji anaweza kukopa kulingana na uwino wa akiba yake na kupewa muda wa marejesho kwa muda wa miaka mitano.
“Saccos hii ipo kwa ajili ya kumsaidia mteja na kuhakikisha muda wote anapata huduma bora kwa wakati, tumeona wananchi wengi wanateseka na mikopo ya kausha damu ambayo wanapewa riba kubwa kwa kila siku” amesema Bi. Lukanga.
Amesema kuwa Saccos hiyo imekuwa msaada kwa wafanyakazi wengi kwa uendelee kutekeleza majukumu yao bila kuwa kikwanzo kwani imekuwa sehemu ya tulizo la moyo wao.
Amesema Hazina Saccos imekuwa na utamaduni wa kumuangalia mwanachna ana uhitaji gani na kumpatia fursa, kwani baadhi ya wanachama Mkoani Dodoma waliwapatia mkopo na viwanja kwa ajili ya kujenga makazi.
Amefafanua kuwa hazina saccos inapokea wanachama Tanzania Bara wanaofanya kazi katika katika ofisi za Serikali.
Amesema kuwa kujiunga na hazina Saccos Sh. 50,000 pamoja kuweka hisa ya Sh. 500,000 ambapo baada ya kujiunga wanachama mpya anakaa kwa muda wa miezi mitatu ili aweze kupata huduma ya mkopo.
Hazina Saccos imefanikiwa kuwa na wanachama wengi ikiwemo viongozi wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.