Na. Gibson G. Bayona
Wakati tunashuhudia mapokezi makubwa ya Ndg. Paul Makonda katika majukumu yake mapya Katika uchambuzi huru ni wazi na bayana kuwa Kuna viongozi wana nyota kali sana katika ulimwengu wa Uongozi na hata iweje au iwe nini watu wanakua na shauku ya kujua wapo wapi, wanafanya nini, wanasema nini, wanawaza nini na wanatamani kuwaona wakiwa in action wazidi kuwafaidi kwa lolote lile.
Jambo kubwa sana ni kuwa viongozi wa aina na hata mapito yao yaweje kwenye safari yao ukweli unabaki kuwa wanayo bahati hiyo na wanafanikiwa sana kwa mapokeo kwa jamii..!
Huyu ni mmoja Ndugu Makonda ni mmoja wa Viongozi hawa hapa Nchini.
Nikipigilia msumari kabisa niseme Hii ni ya asili na kamwe hailazimishwi na wala haizuiliki, ni inborn na ni Gift.!
Upande wa pili ni kwamba, huyu ni kiongozi wa Chama, waliompokea kwa Shangwe ni wananchama wa Chama hicho, waliompa nafasi ni katika Muktadha wa Chama, ina maana Chama kimepiga hesabu zake kimeona kitafidi nini ndani yake na kitafaidika kwelikweli kwani kazi ya Chama ni vita ya kushinda uchaguzi na kushika Dola na katka hilo silaha yoyote ile inatumika na hii kwasasa ni Silaha imara ya kuifanya kazi hii.
Mwisho nimetumia picha hii kiongozi huyu akiingia na Bodaboda na akiendesha mwenyewe; Amini usiamini tayari kabla hajafungua kinywa chake imetosha kuleta mjadala mzito.
Jambo kubwa nililojifunza kwa mwanasiasa Mahiri na mwanadiplomasia Makini anaetenda sana zaidi kuongea sana (Maneno dhidi ya Matendo) Rais wetu na M/Kiti wa CCM Taifa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan jambo muhimu kwake ni kufanikisha adhma yake ya kuifanya kazi yake kwa mafanikio,l na amejipanga vizuri katika hatua muhimu ikiwa ni pamoja na kukiimarisha chama chake ili impunguzie pia kazi upande huu muhimu wa Utekelezaji wa Ilani na kuhiimarisha sana Chana na kinapokua Imara yeye aendelee kupambana na Taifa letu ambalo linauhitaji mkubwa sana na changamoto; Mwisho wa Siku ameshinda na atafanikiwa.
Chaguo limekuwa sahihi chama kitachangamka ZAIDI na siasa itanoga kwasababu katika Taasisi hata iweje nafsi ina nafasi kubwa ya kuchagiza hatma yake hata kama kiuhalisia Taasisi inatakiwa kubaki kuwa kubwa zaidi ya nafsi na ndivo ilivo kwa Chama ila uwepo wa watu wanaotoa mchango wao kwa vipawa vyao huichangamsha Taasisi na kuionogesha, ni kama chumvi kwenye mboga..