……..,………….
Makumbusho ya Taifa la Tanzania na Makumbusho na Mambo ya Kale Zanzibar zImesaini mkataba wa mashirikiano katika uhifadhi wa malikale nchini.
Mkataba wa mashirikiano baina ya makumbusho hizo umesainiwa tarehe 25 Oktoba 2023 na wakuu wa Taasisi hizo mbili.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga alisaini mkataba huo kwa niaba ya taasisi yake na kwa upande wa Zanzibar Mkataba huo ulisaini na Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale, Bi Maryam Mansab.
Katika mkataba huo wa mashirikiano taasisi hizo zimekubaliana kushirikiana katika maeneo ya uhifadhi, utafiti, utalii wa malikale, utoaji elimu kwa jamii, mafunzo na kujenga uwezo kwa watumishi na kufanya matukio na maonesho ya pamoja.
Aidha, viongozi wa wizara walishuhudia utiaji saini huo akiwepo Dkt. Amina Amer, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar na Bw. Bernard Patrick, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbas.