Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul -Razaq Badru akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika mkutano ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambao umefanyika leo Oktoba 26, 2023 Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Daudi Kosuna akizungumza katika mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambao umefanyika leo Oktoba 26, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakiwa katika mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambao umefanyika leo Oktoba 26, 2023 Jijini Dar es Salaam
Wahariri wa Vyombo vya Habari wakiwa katika mkutano na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambao umefanyika leo Oktoba 26, 2023 Jijini Dar es Salaam
………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imefanikiwa kukusanya jumla shilingi trillion 1.34 kati ya shilingi trillion 2.1 kutoka kwa wanufaika wa mikopo kiwango ambacho sawa na asilimia 64.
Akizungumza leo Oktoba 26, 2023 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul -Razaq Badru, amesema kuwa mpaka sasa kuna jumla ya wanufaika 754, 000 ambao wamesoma kwa fedha ya serikali.
Bw. Badru amesema kuwa katika utekelezaji wa marejesho ya mikopo ya wanufaika bado kuna kiasi shillingi bilioni 758 ambacho wanufaika hawajarejesha.
“Tunaendelea kuwafatilia wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ili waweze kulipa na zitumike kwa wahitaji wengine” amesema Bw. Badru.
Bw. Badru amesema kuwa katika utoaji wa mikopo hakuna upendeleo wowote, kwani unafatwa kanuni na taratibu ambazo zimeweka katika kuwapatia wanufaika mikopo yao.
Amesema kuwa wakati umefika kwa watanzania kutoa ushirikiano ili kuwapata wanufaika na kuanza kurejesha fedha hizo.
Bw. Badru amesema kuwa serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa rasilimali watu kwa kuendelea kutoa mikopo kwa ajili ya kusomesha watanzania, hivyo waajiri wanapaswa kuunga juhudi za kuhakikisha waliokopeshwa wanarejesha mikopo hiyo.
Bw. Badru amesema kuwa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa sasa mifumo yao imeunganishwa na mifumo mama ya Taifa kwa ajili ya kuongeza ufanisi ili kufikia malengo tarajiwa.
“Mwaka huu kuna wanufaika 230,000 katika product tatu za under – graduate, diploma na semi scholar ambapo hii ni namba kubwa ya wanufaika ambao wameguswa na fedha zilizopo” amesema Badru.
Bw. Badru amesema kuwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) imeendelea kuwabeba katika kutoaji huduma na taarifa kwa jamii.
Nae Afisa Uhusiano Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Sabato Kosuri, amesema kuwa ofisi ya msajii wa hazina inaendelea kusimamia mslahi ya serikali kwenye taasisi za umma.
Amesema kuwa watanzania wanamatarajio makubwa na taasisi za serikali katika kuhakikisha wanatoa huduma bora na rafiki kwa maslahi ya Taifa.
“Ofisi ya Msajili wa Hazina kupitia maono ya Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu aliona kuna changamoto kwa haya mashirika na taasisi kwamba yanafanya mambo mazuri lakini hayafahamiki” amesema Kosuri.
Amefafanua kuwa ni fursa kwa taasisi za umma kupitia mikutano ya wahariri wa vyombo vya habari kusema malengo, mafanikio pamoja na changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.