O.01:-Katibu UWT Mkoa wa Magharibi Kichama Salama Fadhil Juma akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusiana na ziara ya Mwenyekiti wa UWT Taifa na wajumbe wa kamati tekelezaji Taifa UWT kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi itakayofanyika Oktoba 29 mkoani humo kuelekea sherehe za kumpongeza Dkt.Mwinyi kwa kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake.
Mjumbe wa kamati ya habari ya ziara ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Nafisa Madai Ali akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusiana na ziara yaMwenyekiti huyo na wajumbe wa kamati tekelezaji Taifa (UWT) kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi itakayofanyika Oktoba 29 mkoani humo kuelekea sherehe za kumpongeza Dkt.Mwinyi kwa kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake.
……….
Na Imani Mtumwa Maelezo 26/10/2023
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Marry Pius Chatanda anatarajia kufanya ziara yake katika Mkoa wa Magharib kichama.
Hayo yamesemwa na Katibu mtendaji UWT Mkoa wa Magharibi kichama Salama Fadhil Juma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara hiyo huko ofisini kwake Mwera Wilayani.
Amesema katika ziara hiyo inayotarajiwa kufanyika Oktoba 29 Mwenyekiti wa UWT atatembelea majimbo yote yaliyomo katika mkoa huo na kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo.
Akiyataja majimbo hayo alisema ni pamoja na jimbo la Mwanakwerekwe ambapo wataenda kuangalia maendeleo ya ujenzi wa soko la Mwanakwerekwe na Hospitali ya Wilaya ilipo Kwerekwe Jitimai.
Aidha Mwenyekiti huyo atakagua mradi wa maji safi na Salama katika Jimbo la Dimani eneo la kwearara pamoja na mradi wa nyumba za Mkopo Nafuu Viwanja vya Magereza Tomondo.
Aidha alifahamisha kuwa katika mkoa huo kichama kuna majimbo kumi ambayo wameyagawiwa katika sehemu tano ili kuhakikisha kila Jiimbo linapata nafasi ya kupitiwa na kuangaliwa utekelezaji wa ilani ya chama na mafanikio yaliyofikiwa katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais Mhe Dk.t Hussein Ali Mwinyi.
Kwa upande wake Katibu wa siasa na uwenezi Msekwa Muhammed Ali Mkoa wa Magharib Kichama amesema ziara hiyo imeelekezwa mkoa wa Mjini kwani ndio mkoa uliobeba mambo mbali mbali ya kimaendeleo.
Ziara hiyo ya siku moja itajumuisha wajumbe wa kamati tekelezaji Taifa UWT Mkoa wa Magharibi kichama ikiwa ni shamrashamra za kuelekea kusherehekea utekelezaji wa Dkt.Mwinyi katika miaka mitatu ya uongozi wake.