Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa, (STAMICO) Dk. Venance Mwasse ametoa wito kwa wawekezaji kutoka ndani ya nje ya nchi kuja kuwekezaji kutokana na mazingira rafiki yanayoendelea kuwekwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Dk. Mwasse ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 25 Oktoba 2023 wakati akichangia mada katika kongamano la kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania linalofanyika jijini Dar es salaam.
Dkt. Mwasse Amesema kutokana na jitihada zinazofanywa na Rais Samia katika kuiboresha sekta ya madini Shirika kwa sasa limejengewa uwezo katika nyaja mbalimbali ikiwamo kuwa na Mitambo ya Kisasa ya uchorongaji wa miamba migodini. “Kwa hiyo ninawakaribisha sana tuje tushirikiane na kila mmoja atafaidika kulingana na mazingira bora yaliyowekwa.
“Aliongeza kwa kusema kwa sasa tunafanya kazi na Kampuni ya Anglogold Ashanti katika shughuli za uchorongaji wa miamba na tuna hisa katika umiliki katika mgodi mpya wa Dhahabu wa Buckreef ambao ulianzishwa mwaka jana na kwa sasa umekuwa chachu katika maendeleo ya sekta ya madini nchini,” amesema.
Tanzania ni nchi iliyojaliwa aina mbalimbali za madini ikiwamo Madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee.
Mkutano huo ni wa siku mbili na umenza leo tarehe 25 Oktoba 2023 na unalandana na Kauli mbiu isemayo “Unlocking Tanzania’s Future Mining Potential”. Kaulimbiu hiyo imelenga kuweka mazingira yatakayowezesha kuvuna madini yaliyopo Tanzania kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mkutano huu umefunguliwa rasmi Leo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Biteko