Mhasibu Mwamdamizi wa Serikali Kitengo Cha Pesheni, Wizara ya Fedha CPA. Jenipha Josephat akiwasilisha mada katika Kongamano la wanamitandao ya kijamii na wizara ya Fedha lililomalizika Leo mjini Jumanne Oktoba 24, 2023 Morogoro.
………………………
NA JOHN BUKUKU, MOROGORO
Wizara ya Fedha imefanya maboresho makubwa ya Teknolojia katika mfumo wa ulipaji wa Pensheni ili kuhakikisha wastaafu wanapata huduma bora na ufanisi wakiwa maeneo yote nchini.
Akizungumza leo Oktoba 24, 2023 Mkoani Morogoro kuhusu mfumo wa kielekroniki wa malipo ya Pensheni kwa wastaafu mara baada ya kutoa mada kwenye semina ya wamiliki wa mitandao ya kijamii, Mhasibu Mwamdamizi wa Serikali Kitengo Cha Pesheni, Wizara ya Fedha CPA. Jenipha Josephat, amesema kuwa amesema kuwa Wizara inaendelea kuboresha mfumo wake wa ulipaji kwa kutumia teknolojia ili kuongeza ufanisi.
CPA. Josephat amesema wamekuwa wakiboresha huduma zao kwa ajili ya kutoa huduma kwa wastaafu ili kuondoka usumbufu wakati wakipata huduma.
“Watumishi wa Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na kitengo cha Pensheni wametengeneza mfumo wa malipo kwa njia ya teknolojia ili wastaafu wanaolipwa na wizara wapate huduma katika mikoa yote ambapo kuna ofisi ndogo ya hazina” amesema CPA. Josephat.
Amesema kuwa mfumo huo unapatikana katika ofisi zote za hazina zilizopo bara na viziwani ambapo mstaafu anaweza kupata huduma bila kufika makao mkuu ya nchi Jijini Dodoma.
CPA. Josephat amesema kuwa Wizara ya fedha inajukumu la kutoa huduma ya Pensheni kwa wastaafu ambao wakati wanastaafu kulikuwa hakuna huduma ya kuchangia katika mfuko wa hifadhi ya jamii.
Amesema kuwa wastaafu wanaolipwa ni wale waliostaafu wakati mfuko wa hifadhi ya jamii haijaaza kufanya kazi mwaka 2004.
“Mtu yoyote aliyestaafu baada ya mfuko ya hifadhi ya jamii kuanza kuchangia huyo hausiki katika mpango wa wizara ya fedha” amesema CPA. Josephat.