Katibu Mkuu Ofisi ya Mkamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiongoza kikao cha Kamati Tendaji ya Mradi wa Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (NAP) kilichofanyika jijini Dodoma leo Oktoba 24, 2023.
Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akichangia wakati wa Kikao cha Kamati Tendaji ya Mradi wa Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (NAP) kilichofanyika jijini Dodoma leo Oktoba 24, 2023
Mratibu wa Mradi wa Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (NAP) Bi. Asia Akule kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Septemba 2023 wakati wa Kikao cha Kamati Tendaji kilichofanyika jijini Dodoma leo Oktoba 24, 2023.
Mwakilishi wa Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania Amon Manyama akizungumza wakati wa Kikao cha Kamati Tendaji ya Mradi wa Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (NAP) kilichofanyika jijini Dodoma leo Oktoba 24, 2023.
Washiriki wakiwa katika Kikao cha Kamati Tendaji ya Mradi wa Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (NAP) kilichofanyika jijini Dodoma leo Oktoba 24, 2023.
…………..
Katibu Mkuu Maganga ahimiza ufanisi Mpango wa Kuhimili mabadiliko ya tabianchiKatibu Mkuu Ofisi ya Mkamu wa Rais Bi. Mary Maganga amewahimiza viongozi wote wanaosimamia Mradi wa Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (NAP) kufanya kazi ipasavyo na kwa usahihi.
Ametoa wito huo wakati akiongoza kikao cha tatu cha Kamati Tendaji ya NAP cha mwaka cha kupitia taarifa za utekelezaji wa mradi kuanzia Aprili hadi Septemba, 2023.
Amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa kasi ili kukimbizana na muda huku akisisitiza kuwa katika kikao kijacho kila mmoja awe ametekeleza vyema majukumu yake kama ilivyokubalika.
“Kila jambo lina changamoto zake lakini hadi hapa tulipofika sasa tumeona mafanikio makubwa tangu tulipoanza utekelezaji wa mradi huu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali,” amesema Bi. Maganga.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi huo, Bi Asia Akule kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais amesema hadi sasa utekelezaji wa mradi unakwenda vyema na kwa mafanikio makubwa.
Amesema unatekelezwa kwa kujenga uwezo wa utayari wa nchi katika kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia Mpango wa Taifa wa kuhuisha masuala ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mradi huo wa miaka mitatu ulianza kutekelezwa mwaka 2022 na utafikia tamati mwaka 2024 ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) inaendelea kutekeleza NAP.