Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Benjamin Kuzaga akiwa na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkaguzi wa Polisi Lovenes Mtemi alifanya ziara katika Shule ya Msingi Azimio iliyopo Jijini Mbeya na kutoa elimu kwa wanafunzi wa darasa la nne kuhusiana na masuala ulinzi na usalama.
Akizungumza na wanafunzi hao, Kamanda Kuzaga amewataka kujiepusha na makundi yasiyofaa na badala yake wajikite katika masomo kwa kuhakikisha wana somo kwa bidii na kufaulu.
Aidha, Kamanda Kuzaga amewataka wanafunzi hao kutokaa kimya dhidi ya vitendo vya uhalifu na kuwasisitiza kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu kwa walimu, wazazi na Jeshi la Polisi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.