Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi COSTECH , Bw. Immanuel I Mgonja kushoto akiwa na Mratibu Mkuu wa Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi wa Vyuo Vikuu (HEET) na Afisa Mratibu Mkuu wa Utafiti toka COSTECH, Dk. Hulda Gideon wakikata utepe kuashiria usinduzi wa magari mapya ambapo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) tarehe 23 Oktoba , 2023 imepokea magari mawili ambayo yatafanya kazi mbalimbali za COSTECH. Magari hayo yamenunuliwa kupitia Mradi wa HEET unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.