Baadhi ya wanifaika wa TASAF wilayani Mkinga mkoani Tanzania.
………………………….
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imefanikiwa kutoa zaidi ya Shilingi bilioni nne (4) kwa mwaka 2013 katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga kwa ajili ya kusaidia Kaya Maskini.
Akizungumza Wananchi hivi karibuni katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, amesema kuwa fedha hizo zimekwenda moja kwa moja kusaidia wakazi wa Wilaya hiyo ili kuondoka na umaskini.
Mhe. Simbachawene amesema kuwa pia imefanikiwa kutumia zaidi ya milioni 900 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Mkinga, huku milioni 210 zikitumika kwa ajili kutoa ajira ya muda mfupi katika kutekelezaji wa miradi.
“TASAF ni mradi wa serikali, hivyo naomba tuisimamie katika utekelezaji wake kama ilivyo katika miradi mengine ili kuhakikisha tunafikia malengo husika” amesema Mhe. Simbachawene.
Mhe. Simbachawene amewataka Watendaji katika Wilaya ya Mkinga kusimamia vizuri katika utekelezaji wa miradi ikiwemo kuhakikisha watu wanaopata kazi katika ujenzi wa miradi wanatoka katika kaya maskini katika Wilaya hiyo.
“Wanaotakiwa kufanya kazi katika utekelezaji wa miradi wawe wamekizi vigezo na kanuni, afya njema na utaratibu unawaruhusu, vijana wanaotoka katika kaya maskini waje kufanya kazi katika hii miradi” amesema
Mhe. Simbachawene.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati alipofanya ziara kuwatembelea wanufaika wa TASAF katika wilaya ya Mkinga mkoani Tanga hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akiendelea na ziara yake wakati alipowatembelea wanufaika wa TASAF katika wilaya ya Mkinga mkoani Tanga hivi karibuni.