Dodoma
Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kazi wanazoendelea kufanya katika maeneo mbalimbali nchini.
Mhandisi Mativila ametoa pongezi hizo wakati alipokutana na kufanya kikao na Menejimenti ya Wakala huo kwenye ukumbi wa TARURA uliopo mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma.
Mhandisi Mativila ameitaka Menejimenti hiyo kusimamia kazi kwa weledi na kuhakikisha kazi zote zinakamilika kwa wakati.
Aidha, amesisitiza matumizi ya teknolojia mbadala kwenye ujenzi wa madaraja ya mawe kwa lengo la kufikisha huduma kwa wananchi na kwa gharama nafuu.
TARURA inaendelea na kazi ya ujenzi,ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara za wilaya zenye urefu wa Kilomita 144,429.77 nchi nzima lengo ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanazifikia huduma za kijamii na kuweza kusafirisha mazao na bidhaa zao kirahisi.