Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akipata maelezo kutoka kwa Mratibu Baraza la Kiswahili Zanzibar Hassan Khamis Saghir kuhusiana na vitabu vya fasihi wakati akitembelea maonesho ya kazi za fasihi katika Tamasha la kwanza la Vitabu lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idris AbdulWakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafasihi Zanzibar ( ZBF) Ally Baharoon akitoa maelezo kuhusiana na Tamasha la kwanza la Vitabu lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idris AbdulWakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Mshindi wa tuzo za Fasihi mwaka 2021 Prof.Abdulrazak Gurnah akizungumza kuhusu Dunia ya uwandishi katika Tamasha la kwanza la Vitabu lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdul Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Mfasiri wa Vitabu Dkt.Ida Hadjivayanis kutoka Chuo Kikuu cha London Akizungumza kuhusu ladha ya vitabu katika Tamasha lakwanza la Vitabu lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdul Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Washiriki wa Tamasha la kwanza la Vitabu wakifuatilia tamasha hilo lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idris AbdulWakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said Akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha PEPONI kilichoandikwa na Prof.Abdulrazak Gurnah na kutafsiriwa na Dkt.Ida Hadjivayanis katika Tamasha la kwanza la Vitabu lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdul Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza wakati akizundua tamasha la kwanza la Vitabu lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdul Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Waziri wa Nchi (OR) Fedha na Mipango akizungumza katika Sada Salum Mkuya uzinduzi wa tamasha la kwanza la Vitabu lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdul Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
……..
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said amewataka waandishi wa Vitabu kuuhifadhi utamaduni wa Mzanzibari ili uweze kurithiwa na vizazi vijavyo.
Ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa tamasha la kwanza la Vitabu vya Zanzibar katika ukumbi wa Idrisa Abdulwakil Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Amesema ni muhumu kwa waandishi kuuendeleza Utamaduni wa Mzanzibari unaohamasisha umoja na upendo badala ya kuchochea vurugu jambo ambalo ni kinyume na malengo ya Vitabu hivyo.
Amesema Zanzibar ni kitovu cha Fasihi bora na imetoa waandishi mashuhuri ambao wamejipatia umaarufu Duniani na hivyo kusaidia kuitangaza Zanzibar.
Aidha, meishukuru Jumuiya ya Vitabu Zanzibar (ZBF) kwa maandalizi mazuri ya Tamasha hilo na kuahidi kuwa Serikali italiendeleza na kulikuza kwani linaongeza idadi ya Matamasha yanayoitangaza Zanzibar Kimataifa.
Naye Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Saada Mkuya Salum amesema ni vizuri kwa waandishi wa vitabu kutuma vitabu hivyo mtandaoni kwani kufanya hivyo itakuwa ni rahisi kuwafikia wasomaji wengi ili lengo la vitabu hivyo liweze kufikiwa.
Naye Mkurugenzi wa Jumuiya ya Vitabu Bw. Ally Baharoon amesema Tamasha hilo ni muhimu kwani litachangia kuwakutanisha waandishi wa ndani na waandishi wa kimataifa ili kujengeana uzoefu katika kazi zao za utunzi wa vitabu vyao.
Ndg, Bahroon amesema Vitabu ni hazina nzuri inayoweza kudumu na kurithisha elimu, huruma, na mahusiano mema kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Ufunguzi wa Tamasha hilo la siku tatu limehudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Mabalozi, Mshindi wa Tunzo ya Fasihi ya Nobel Profesa Abdulrazak Gurnah na waandishi mbali mbali wa Vitabu kutoka Zanzibar nan je ya Zanzibar ambapo kauli mbiu ya Tamasha hilo ni “ULIMWENGU NDANI YA MANENO”