Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka nchini Kenya Nyamari Ongegu Maarufu kwa jina la Nyashinski akiwasili Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage kwa ajili kutoa burudani katika Tamasha la Serengeti Lite, Oktoba Festival linalotarajia kufanyika kesho Oktoba 21, 2023 katika fukwe za Coco, Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka nchini Kenya Nyamari Ongegu Maarufu kwa jina la Nyashinski akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam kuhusu ushiriki wake katika Tamasha la Serengeti Lite, Oktoba Festival linalotarajia kufanyika kesho Oktoba 21, 2023 Coco Beach.
Meneja Mawasiliano Uendelee Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) Bi. Rispa Hatibu (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo na Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka nchini Kenya Nyamari Ongegu Maarufu kwa jina la Nyashinski baada ya kuwasili katika Viwanja vya ndege vya Kimataifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka nchini Kenya Nyamari Ongegu Maarufu kwa jina la Nyashinski amewasili leo Oktoba 20, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage kwa ajili kutoa burudani katika Tamasha la Serengeti Lite, Oktoba Festival linalotarajia kufanyika kesho Oktoba 21, 2023 katika fukwe za Coco, Dar es Salaam.
Katika Tamasha la Serengeti Lite, Oktoba Festival maelfu ya watu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki wanatarajia kushiriki, huku zaidi ya watu 500 wanatarajia kupata fursa mbalimbali ikiwemo uchumi na biashara.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Msanii wa mukizi Nyashinski, amesema kuwa anafurai kubwa kushiriki katika Tamasha Serengeti Lite, Oktoba Festival, huku akiahidi kutoa burudani kabambe kwa washiriki wa Tamasha hilo.
“Ni Tamasha kubwa, najiona msanii mwenye bahati ya kupata nafasi ya kushiriki na wasanii wakubwa wenye majina na heshima kama Ali Kiba na Jose Chameleon, ambapo nashiriki nao katika Jukwaa moja” amesema Nyashinski.
Nyashinski amesema kuwa anatarajia kuimba nyimbo zote pendwa katika Tamasha, huku akibainisha “Nina nguvu za kutosha katika kuhakikisha natoa burudani kabambe”.
Katika hatua nyengine amefafanua anatarajia kufanya korabo na baadhi ya wasanii nchini Tanzania ili kuhakikisha muziki wa ukanda Afrika unaendelea kupiga hatua.
Tamasha la Serengeti Lite, Oktoba Festival limekusudia kuinua vipaji vya watanzania pamoja kuongeza fursa mbalimbali ikiwemo uchumi.
Wadau mbalimbali wa maendeleo wameshauri kuwekeza ili waweze kuinuka vipwa vya watanzania kama wanavyofanya Kampuni Serengeti Breweries (SBL).