Uongozi wa Benki ya NMB kanda ya kusini ukiongozwa na Meneja wa Benki hiyo Bi.Faraja Raphael Octoba 19,2023 wameunga jitihada za ujenzi wa zahanati ya Polisi Kwa kukabidhi vifaa vyenye thamani ya TSH,Million kumi na Saba.(17,000,000/=) .Vifaa vilivyo kabidhiwa ni pamoja na Bati, Mbao, Misumari ya Bati pamoja na Kofia za Bati.Pia Bi. Faraja ameupongeza uongozi wa Jeshi la Polisi Tanzania Kwa kua jirani na Benki ya Nmb Kwa kushirikiana katika Mambo mbalimbali na ushirikiano huo ndio unaifanya Benki yetu kuwa imara.
Pia kama wadau tunao wajibu wa kuunga juhudi za maendeleo katika Jamii.
Kwa upande wake Mgeni Rasm Mh, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi. Mwanakhamisi Mkundi amemshukuru Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara ,watumishi wa serikali pamoja na menejimenti ya Nmb Kwa kuungana kuja kupokea msaada huo.
Bi mwanakhamisi amesema utamaduni huu wa Benki ya Nmb kushiriki katika Shughuli za maendeleo ya kijamii pia ushirikiano huu unatokana na malezi Bora wanayo yapata kutoka Kwa serikali.
Bi. Mwanakhamis amesisitiza kuwa sekta ya Afya ni miongoni mwa sekta ambayo imepewa kipaumbele na serikali ya awamu ya sita.ameendelea kulipongeza Jeshi la Polisi Kwa kusogeza huduma Kwa Jamii na amehaidi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Kwa kipindi chote ambacho amepewa dhamana na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hafla ya kukabidhiwa vifaa hivyo ilihudhuriwa na Afisa mnadhimu namba Moja wa kikosi Cha Afya Tanzania Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Dkt.Suleiman ambaye pia ni mtaalamu wa magonjwa ya akina mama ameishukuru Benki ya Nmb na kusisitiza sote tuungane kumvusha mama na mtoto salama na amehaidi kulitendea haki jengo ambalo litajengwa .
Akipokea vifaa hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Nicodemus Katembo ameishukuru Kwa dhati Benki ya NMB Kwa kuunga juhudi ya ujenzi wa Jengo la wodi ya mama na mtoto na kusema kuwa Zahanati hiyo ilianza kujengwa Kwa nguvu za ndani kupitia mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na kusisitiza kua Zahanati hii inahudumumia Askari pamoja na Raia na ni miongoni mwa Zahanati inayoongoza Kwa kujali wagonjwa pamoja na kutoa huduma Bora Kwa Jamii.
Acp Katembo alihitimisha kwa kusema msaada huu utatufikisha kufikia lengo la kupata Kituo Cha Afya kabla au ifikapo Mwaka 2025, sambamba na hilo amewataka Wananchi na taasisi zingine kuendelea kuungana Ili kumvusha mama na mtoto salama.