………………..
Na Sixmund Begashe
Mahafali ya Kozi namba 72 ya Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) yanatarajiwa kutoa elimu Uhifadhi kwa wote wakatao hudhuria tarehe 21 Oktoba 2023, kwa kuwa maandalizi yake yanasehemu ambazo zitatoa fursa kwa jamii kujifunza mbinu mbalimbali za kudhibiti Wanyamapori wakali na waharibifu kwenye maeneo yao.
Akizungumza baada ya kukagua maandalizi ya mahafali hayo, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii ( CBCTC) – Likuyu Sekamaganga, Bi. Jane Nyau, amesema maandalizi yamekamilika na Askari hao wapo tayari kuhitimu Mafunzo yao, hivyo ametoa wito kwa jamii kuhudhiria kwa wingi ili waweze kunufaika licha ya gwaride kutoka kwa VGS hao pia watapata nafasi ya kujifunza mambo muhimu ya Uhifadhi wa Maliasili.
Bi. Nyau mamebainisha kuwa, Mafunzo hayo ya VGS 114 ambayo yamedhaminiwa na Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Nyanda za juu Kusini (REGROW), yatafungwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna Benedict Wakulyamba, Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.