Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA. Habib Suluo akizungumza katika kikao kazi na Ofisi ya Msajili wa Hazina na Jukwaa la Wahariri Tanzania kilichofanyika leo Oktoba 19, 2023 kwenye ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam.
‘
Mkurugenzi wa barabara kutoka LATRA, Johansen Kahatano akifafanua baadhi ya mabo katika kikao kazi na Ofisi ya Msajili wa Hazina na Jukwaa la Wahariri Tanzania kilichofanyika leo Oktoba 19, 2023 kwenye ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam.
…………………………….
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imefanikiwa kuongeza mapato katika utendaji wa kazi kutoka shilingi bilioni 25.95 kwa 2020/202, bilioni 28.53 kwa mwaka 2021/2022 hadi kufiki bilioni 34.17 kwa mwaka 2023.
Akizungumza katika kikao kazi na Ofisi ya Msajili wa Hazina na Jukwaa la Wahariri Tanzania kilichofanyika leo Oktoba 19, 2023, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA. Habib Suluo, amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na kufanya kazi kwa ufanisi katika kutoa huduma bora kwa jamii.
CPA. Suluo amesema kuwa wamefanikiwa kuongeza mapato kwa asilimia 10 kutokana na ushirikiano mzuri wanaopata kutoka kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassan.
“LATRA ni taasisi inayojitegemea na tumejipanga kufanya kazi kwa ufanisi katika udhibiti wa mambo mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yetu” amesema CPA. Suluo.
CPA. Suluo amesema kuwa hawajawahi kupata hati chafu miaka yote ya utendaji kazi kutokana na umakini katika utendaji kazi.
“Tumefanikiwa kufungua ofisi katika mikoa yote ya Tanzania ili kuwa karibu na wananchi jambo ambalo litasaidia kuendelea kutoa huduma bora” amesema CPA. Suluo.
Ametoa wito kwa wadau mbalimbali kufanya kazi kwa ushirikiano na LATRA
ili kufikia malengo ya kuendelea kutoa huduma bora ambayo yamewekwa na serikali ili kuwapa wananchi huduma iliyo bora kabisa.
Mkurugenzi wa Reli Wakala wa Usafiri wa Ardhini LATRA Mhandisi Hanya Mbalawa akiwasilisha mada kuhusu mambo ya uendeshaji wa Reli katika kikao kazi na Ofisi ya Msajili wa Hazina na Jukwaa la Wahariri Tanzania kilichofanyika leo Oktoba 19, 2023 kwenye ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Neville Meena akifafanua baadhi ya mambo wakatika wa kikaokazi hicho.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Ofisi ya Masajili wa Hazina Bw. Sabato Kosuri wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.