Makamanda wa Polisi kutoka Mikoa ya Kanda ya ziwa (waliosimama) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi wakwanza kushoto ni Makamu mwenyekiti.
Wakuu wa oparesheni,wakuu wa upelelezi na wadau wa uvuvi wakiwa kwenye kikao Jijini Mwanza.
……….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Kanda ya ziwa,wakuu wa upelelezi,wakuu wa oparesheni pamoja na wadau wa Sekta ya uvuvi wamekutana Jijini Mwanza kwa lengo la kupokea taarifa ya tathimni ya kikao kilichofanyika Aprili mwaka huu Mkoani Geita juu ya mikakati ya muda mfupi,wakati na mrefu wa kuzuia na kupamba na uhalifu katika ziwa Victoria.
Kikao hicho kimefanyika leo Jumatano Oktoba 18, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu Jijini Mwanza
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa vikosi maalumu vya oparesheni ndani ya Jeshi la Polisi Ferdinand Mtui amesema, kikao hicho ni cha tano na kitatoa tathimni ya vikao vilivyopita huku akieleza mikakati watakayoiweka itasaidia kuzuia na kupamba na uhalifu ili kuweza kuwapa wananchi fursa ya kufanya shughuli zao kwa uhuru na amani.
Mtui alisema kuwa kwa sasa uhalifu ndani ya ziwa Victoria umepungua kwa kiasi kikubwa sana na hii ni kwasababu ya ushirikiano uliofanyika kati ya Jeshi la Polisi,vyombo vya ulinzi na usalama,wadau wa uvuvi pamoja na wananchi wanaolizunguka ziwa hilo.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti kamati ya uvuvi endelevu Ziwa Victoria Hassan Muhenga amesema tangu kuanza kwa vikao hivyo kunamabadiliko makubwa kwani uhalifu wa ziwani umetoweka japo bado kunauhalifu wa wavuvi kwa wavuvi wa kunyanganyana zana za uvuvi.
Awali akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amesema Sekta ya uvuvi ni miongoni mwa sekta muhimu inayochangia kuondoa umasikini na kukuza uchumi katika Mkoa wa huo na Taifa kwa ujumla.
“Kwamujibu wa takwimu sekta ya uvuvi inachangia asilimia saba katika pato la Mkoa wetu wa Mwanza na tasnia hii ya uvuvi ni muhimu Katika utoaji wa ajira ya mtu mmoja mmoja wafanyabiashara wakubwa na wakati, wafugaji,chakula na lishe kwenye ngazi ya familia na jamii kwaujumla.