Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Emmanuel Charles maarufu kama Malupelupe (22) mkazi wa Mafisa na wenzake watano kwa tuhuma za wizi za kupola kwa kutumia pikipiki (Vishandu).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP- Alex Mkama amesema mnamo Ocktoba 13, 2023 majira ya saa 4 maeneo ya Mtawala Manspaa ya Morogoro watuhumiwa wakiwa na Pikipiki aina ya Haojue yenye namba za usajili MC 270 DMS walipola simu ndogo aina Tecno yenye thamani ya 30,000 na fedha shilingi 50,000 na baadaye kutiwa mikononi mwa jeshi la Polisi.
Baada ya upekuzi wahutumiwa hao walikutwa na Pikipiki mbili aina ya Haojue zenye namba za usajili MC 270 DMS na MC414CTW ambazo wamekuwa wakizitumia kufanya uharifu.
Pia walikutwa na simu moja ndogo aina ya Tecno, makasha ya simu 13, pochi za kike 16 na simu janja 10 aina mbalimbali ambazo wameziiba kwa nyakati tofauti.
Aidha jeshi la Polisi linatoa wito kwa wazazi na walezi kuwalea vijana wao katika maadili ili kuwaepusha na vitendo vya kiharifu.