Na Ahmed Mahmoud
Waziri wa Katiba na Sheria ,Balozi Dk,Pindi Chana amesema Tanzania itaendelea kuwa mfano Bora kwa utulivu na amani Duniani Kote kutokana na kulinda haki za binadamu na wa Watu katika Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla.
Akizungumzia maandalizi ya mkutano huo unaotarajia kufanyika Oktoba 20 hadi Novemba 9 mwaka huu Jijini Arusha,Balozi Pindi Chana alisema Mashirika mbalimbali yasiyo ya Kiserikali yatahudhuria mkutano huo
“Tanzania itaendelea kuwa mfano bora wa kudumisha haki za binadamu na watu lakini pia hii ni fursa kwa Mkoa wa Arusha nawashukuru wadau wetu kwa kushiriki mkutano huu”
Aliwakaribisha wadau mbalimbali wa haki za binadamu kushiriki mkutano huo na kuweka mikakati kwani haki za binadamu zinapozingatiwa ndio mambo mbalimbali yanaweza kuendelea na kwa Tanzania mnaona mambo yanakwenda vema chini ya uongozi wa Rais Samia Hassan Suluhu
Naye Rais na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Remy Lungu akiongozana na makamishna wengine na watendaji wa tume hiyo wamewasili katika Uwanja cha Ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro (KIA)kwa ajili ya mkutano huo
Kamishna Lungu alisema mkutano huo utajadili masuala mbalimbali yanayohusu haki za binadamu na watu katika nchi za Afrika kwani bado changamoto nyingi za ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi hizo kwenye maeneo mbalimbali.
“Tumekuja kujadiliana juu ya haki za binadamu na tutoke na maazimio ambayo yatawezesha kila nchi kutekeleza ,siwezi sema sana nchi fulani inafanya vema kuliko nyinginezo katika masuala ya haki za binadamu kwakua kila nchi inamatatizo yake”
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu na Watu,Abiola Idowu Ojo alisema tume hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya haki za binadamu na watu katika bara hilo tangu iundwe.
“Michango ni mingi na tunaona haki za watoto,wanawake na umiliki wa ardhi zinazongatiwa na sasa lazima tuanishe changamoto zinazotukanili
Wajumbe zaidi ya 700 kutoka nchi za Afrika wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo jijini Arusha.