Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya Srikanta Pradhan wakivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya Mji wa Shelui katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Kijiji cha Kizonzo, Wilaya ya Iramba Mkoani Singida tarehe 17 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya Srikanta Pradhan pamoja na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso wakati wakivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya Mji wa Shelui katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Kijiji cha Kizonzo, Wilaya ya Iramba Mkoani Singida tarehe 17 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya Srikanta Pradhan wakati akielekea kuzindua mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya Mji wa Shelui katika hafla iliyofanyika kwenye Kijiji cha Kizonzo, Wilaya ya Iramba Mkoani Singida tarehe 17 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi mara baada ya kuzindua mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya Mji wa Shelui katika hafla iliyofanyika kwenye Kijiji cha Kizonzo, Wilaya ya Iramba Mkoani Singida tarehe 17 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungulia Maji mara baada ya kuzindua mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya Mji wa Shelui katika hafla iliyofanyika kwenye Kijiji cha Kizonzo, Wilaya ya Iramba Mkoani Singida tarehe 17 Oktoba, 2023.
Wananchi wa Kijiji cha Kizonzo wakiwa kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya Mji wa Shelui tarehe 17 Oktoba, 2023
Tangi kubwa lenye ujazo wa lita 300,000 likiwa limejengwa katika Kijiji cha Kizonzo kama sehemu ya mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya Mji wa Shelui tarehe 17 Oktoba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Iramba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Shelui katika muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi Mkoani Singida tarehe 17 Oktoba, 2023.
Wananchi wa Shelui pamoja na Vijiji Jirani wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Shelui Mkoani Singida tarehe 17 Oktoba, 2023.