Na Lucas Raphael,Tabora
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku mbili mkoani Tabora itakayoanza Octoba 17 hadi 18 ambapo atatembelea wilaya za Igunga na Nzega, ambako poa atakagua miradi ya chuo cha Veta Igunga na Shamba la mbegu Kilimi wilaya ya Nzega.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian alisema Rais Samia Suluhu Hassan akimaliza ziara mkoani Singida ataaza ziara katika mkoa huo.
Alisema kwamba katika ziara hiyo ataweka jiwe la msingi chuo cha veta wilayani Igunga kilichogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.6 ambacho kimefikia hatua za mwisho kukamilika kisha anatarajiwa kuongea na wananchi katika uwanjwa wa Barafu.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba mara baada ya mkutano huo atakwenda hadi wilaya ya Nzega ambako atatembelea shamba la mbegu Kilimi kuangalia teknolojia ya umwagiliaji iliyofungwa kwenye shamba hilo.
Balozi Dkt. Batilda alisema kwamba sahamba hilo lenye ukubwa wa ekari 1000 limewekewa mitambo hiyo ya umwangiliaji kwa gaharama ya shilingi Bilioni 6.2.
Alisema kufungwa kwa mitambo hiyo kutasaidia shamba hilo kuzalisha mbegu kwa muda wote wa mwaka hivyo kuongeza tija.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Tabora amewataka wananchi wa mkoa wa Tabora kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumpokea Rais Samia.