Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara lina mshikilia Mwanaume mmoja jina limehifadhiwa (56) Muislamu na mkazi wa Kijiji cha Makong’onda wilaya ya Masasi Kwa tuhuma za kumjeruhi mke wake Kwa kumuingizia Panga sehemu ya haja kubwa.
Ni kwamba tukio hilo limetokea tarehe 08.10.2023 majira ya saa 19:00hrs,Kijiji na kata ya Makong’onda wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara.
Ni kwamba mtuhumiwa jina (limehifadhiwa)Pamoja na mhanga baada ya kutoka kwenye mihangaiko yao ya kuokota korosho mhanga alikwenda Kwa Binamu yake kutwanga kisamvu ambapo ni eneo jirani na wanapoishi”
Baada ya kukaa huko Kwa muda mumewe alihisi kua ameenda Kwa Mwanaume mwingine.na ndipo baada ya kurejea alianza kumshambulia Hadi muhanga kupoteza fahamu.
Baada ya hapo mtuhumiwa (Jina limehifadhiwa) alichukua panga na kumuingizia muhanga sehemu ya haja kubwa na kumsababishia majeraha”.
Mhanga wa tukio hili anaendelea na matibabu katika hospitali ya Newala na hali yake inaendelea vizuri.na mtuhumiwa anatarajia kufika mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili.
Aidha kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Nicodemus Katembo ametoa Rai Kwa wananchi Kwa ujumla kuacha kushiriki vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia unao husisha wivu wa mapenzi na hatua Kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya wahalifu dhidi ya vitendo hivi vya kikatili Kwa Jamii zetu