Ikiwa leo ni Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Muasisi wa Taifa hili Hayati Julius Kambarage Nyerere; Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu ameongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama kujionea shughuli mbalimbali zinavyotekelezwa katika Ziwa Ngosi.
Ziwa Ngosi linalosimamiwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) chini ya Hifadhi Asilia ya Mlima Rungwe lina kipenyo cha km 01 na hivyo kuwa moja ya maziwa makubwa Ya asili ya Kivolkano Tanzania na la pili kwa Ukubwa Afrika baada ya lile lililopo nchini Ethiopia.
Mhe Haniu amehamasisha Wakazi wa Rungwe na Tanzania kwa ujumla kutembelea vivutio vilivyopo ikiwa ni hatua ya kufanya matembezi sambamba na kuongeza pato la taifa.
Amesema Wilaya ya Rungwe ina vivutio vingi hivyo kila mmoja anatakiwa kivihifadhi pamoja na kutembelea mara kwa mara ili kujifunza, kuongeza maarifa na hivyo kupata uelewa ambao utakuwa muhimu kwa kizazi hiki na kijacho.
Pamoja na Ziwa Ngosi pia amepanda mlima Rungwe ikiwa ni hatua ya kuhamasisha utalii wa ndani .
Mlima Rungwe una urefu wa Mita 2981 msl na ndio mlima wa tatu kwa urefu Tanzania baada ya Kilimanjaro na Meru na wastani wa watalii 2000 hupanda kila mwaka na hali ya wwe hii imeongeza pato la taifa pamoja kuchangamsha uchumi wa wakazi wanaouzunguka mlima Rungwe