Meneja Masoko wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Sophia Mang’enya akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa droo ya kwanza ya taasisi hiyo. Kampeni hiyo pia itamwezesha mteja wao kushinda simu ya mkononi aina ya Samsung na pikipiki kila wiki kwa wiki nane wakati mshindi wa wiki ya tisa atashinda zawadi ya gari aina ya IST.
Msimamizi kutoka michezo ya Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Salim Magufi akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa droo ya kwanza ya taasisi hiyo Y9 Microfinance. Taasisi ya Y9 Microfinance kwa sasa inaendesha kampeni ambayo itamwezesha mteja wao kushinda simu ya mkononi aina ya Samsung na pikipiki kila wiki kwa wiki nane wakati mshindi wa wiki ya tisa atashinda zawadi ya gari aina ya IST.
Meneja Masoko wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Sophia Mang’enya (katikati) akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa droo ya kwanza ya taasisi hiyo. Kampeni hiyo pia itamwezesha mteja wao kushinda simu ya mkononi aina ya Samsung na pikipiki kila wiki kwa wiki nane wakati mshindi wa wiki ya tisa atashinda zawadi ya gari aina ya IST. Kushoto ni Afisa msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, Salim Magudi na kulia ni Afisa IT wa taasisi ya Y9 Microfinance Reagan Swai
………….
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance, imeanza kumwaga zawadi za washindi kwa wateja wao walioanza kupata huduma tatu tofauti za mikopo.
Katika droo ya kwanza, wateja wawili waliweza kushinda zawadi ya pikipiki na simu ya mkononi aina ya Samsung. Wateja hao ni George Kivuyo ambaye alishinda pikipiki na Ummukulthum Abdallah kutoka Zanziba ambaye ameshinda zawadi ya simu ya mkononi.
Akuzungumza baada ya droo hiyo, Meneja Masoko wa Taasisi ya Y9 Microfinance, Sophia Mang’enya alisema kuwa Kivuyo na Ummukulthum wameshinda zawadi hizo baada ya kukopa kupitia app yao na baadaya kutumia mikopo hiyo, walirejesha mikopo hiyo ndani ya siku tatu kwa mujibu wa taratibu.
Mang’enya alisema kuwa mteja wao anaweza kukopa fedha taslimu, fedha ya malipo ya umeme (LUKU) na muda wa maongezi kwa kutumia ‘app’ yao ambayo lazima uipakue (download).
Alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwanufaisha wateja ambao wamewezesha taasisi hiyo kutimiza mwaka mmoja kwa mafanikio makubwa.
Alisema kuwa kuwa mteja wao anaruhusiwa kukopa kuanzia sh 2,000 mpaka Sh100,000.
“Wateja wanaweza kupata msaada wa kifedha wanavyohitaji kwa haraka zaidi na unachotakiwa kufanya ni kupakua program au App ya Y9 Microfinance na kujiunga ili ufaidike na huduma hizi tatu,” alisema.
Alisema kuwa taasisi ya Y9 Microfinance sio tu inatoa mikopo, bali inawezesha watu kufikia ndoto zao kwa kupitia ubunifu wa hali ya juu na wenye tija.
Aliongeza kuwa ili kuwanufaisha zaidi wateja wao, watachezesha droo kubwa wiki ya tisa ambapo mshindi atazawadiwa gari aina ya IST.
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa michezo ya bodi ya kubahatisha nchini, Bw Salim Bugufi aliipongeza washindi hao na kuwaomba Watanzania kutumia fursa hiyo ili kufikia malengo yao.