Ulinzi wa nchi ni wetu sote hivyo jamii inapaswa kutoa taarifa za vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia na Unyanyasaji dhidi ya Watoto pamoja na kutoa taarifa za Wahalifu na Uhalifu ambao unatokea kwenye himaya zetu ili kuweza kuzishughulikia kwa haraka.
Hayo yamezungumzwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya leo Octoba 13, 2023 katika Msikiti wa Tahadia uliyopo mjini Tunduma mkoani Songwe
Sambamba na hayo Kamanda Mallya alikabidhiwa Quran Takatifu ili aendelee kuhubiri na kukemea uovu, hili limefanyika katika msikiti huo baada ya utoaji wa Elimu juu ya ulinzi na Usalama wa maeneo ya mpakani.
Kwa upande wa waamini wa msikiti huo wamemshukuru Kamanda wa polisi mkoa wa Songwe na wameeleza kuwa kutoa kwake Laki 2 kati ya Laki 5 kwaajili ya kujenga mtalo wa kupitishia maji pindi mvua zinaponyesha litatatua tatizo la kutuama kwa maji katika eneo hilo la msikiti