Serikali kupitia Bohari ya Dawa MSD, imekabidhi Dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 349, 167 kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, kwaajili ya kuboresha utoaji huduma hospitalini hapo.
Akiongea wakati wa kupokea bidhaa hizo, Mfamasia wa hospitali hiyo Bi.Shukuru Robert ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuboresha huduma hospitalini hapo.
Aidha ameipongeza wizara ya Afya chini ya Mhe. Ummy Mwalimu kwa uongozi na usimamizi thabiti wa sekta ya afya.
Bi. Shukuru amebainisha kwamba wamepokea, vitanda vya umeme, Magodoro, Mashuka, Viti vya Magurudumu, pamoja na Dawa aina mbalimbali.