………………….
Na Sixmund Begashe
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba ameridhishwa na kasi ya utekelezwa wa Mradi wa Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Nyanda za juu Kusini (REGROW) katika Hifadhi ya Taifa Ruaha
Alikagua ujenzi wa Miradi hiyo na kuongea na Askari na Maafisa wa Hifadhi hiyo ya pili kwa ukubwa nchini, nakujionea kasi ya ujenzi wa Kiwanja cha ndege, Nyumba za kufikia wageni mbalimbali, Kamishna Wakulyamba amesema miradi hiyo itakapo kamilika itachochea ongezeko zaidi la wageni na kuongeza Pato la Taifa.
Kamishna Wakulyamba ameongeza kuwa, Tanzania sasa inashuhudia matokeo chanya ya kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Filamu ya The Royal Tour, hivyo utekelezwaji wa miradi ya REGROW katika Hifadhi hiyo uendane na kasi ya wingi wa Watalii nchini.
Aidha Kamishna Wakulyamba amesisitiza kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Mhe Waziri Angellah Kairuki itaendelea kutoa ushirikiano kwa wakandarasi wa Miradi hiyo ili wamalize kazi kwa wakati uliopangwa ili iongeze chachu ya kiuchumi kwa watanzania kwa ujumla.
Awali akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Hifadhi ya Taifa Ruaha, Godwell E. Meng’ataki amesema mradi hio unajumuisha ujenzi wa Majengo ya huduma za Utalii na Ulinzi ambapo kwa Hifadhi ya Taifa Ruaha unatekelezwa katika maeneo 6 inatakelezwa na mkandasi Hainan International limited kwa gharama ya Bilioni 17.5.
Ameongeza kuwa ujenzi wa viwanja vya ndege viwili Kiganga na Ukwaheri unatekelezwa na mkandasi CHICO Kwa gharama ya Bilioni 42.1 na kuwa miradi yote inatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 2024
Katika hatua nyingine Kamishna Wakulyamba ametembelea mto wa Ruaha Mkuu na kusikitishwa na hali ya ukame unaosababishwa na shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya mto huo.