Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika kurudisha faida kwa jamii leo Oktoba 12,2023 watoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya milioni tano kwenye Hospitali ya Mnazi moja Zanzibar.
Akizungumza baada ya kutoa vifaa hivyo Afisa Habari na uhusiano wa Shirikia hilo Domina Rwemanyila, amesema kuwa utoaji wa vifaa hivyo ni kurudisha walichokipata kutoka kwao kwani wao wanahudumia jamii.
“Sisi tunakawaida ya kusaidia makundi maalumu, hospitali ya Mnazi mmoja kuna baadhi ya vifaa walituomba tumeona ni wakati sasa wa kuweza kurudisha kwa jamii kwani tumekuwa tukihudumia jamii wakati wote”amesema Rwemanyila.
Amesema kuwa kusaidia hospitali hiyo ni kuongeza ukaribu kati ya Zanzibar na shirika la nyumba pamoja na kusapoti juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Floor Meter, Patients Stand Monitor, Patients Monitor, Pulse Oximeter, Breathing System za Anesthetic Machine na Patients Screen.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar Bw. Abdallah Haji amelishukuru Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kutoa msaada katika hospital hiyo.
Bw. Haji amesema msaada huo ni mwendelezo wa wadau mbalimbali katika kuleta mahitaji katika hospital hiyo.
“Tunafarijika kuona wezetu wanaguswa kwa namna moja au nyengine kushiriki katika utoaji wa huduma kwa wananchi wa Zanzibar” amesema Bw. Haji.
Amesema kuwa wamepokea vifaa mbalimbali ikiwemo vifaa tiba, dawa, chakula pamoja na maji jambo ambalo ni rafiki kwao.