Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza akimsikiliza mratibu wa Maafa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Khowe Malegeri atembelea banda la Ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Wiki ya Kimataifa ya kupunguza madhara ya maafa yanayoendelea katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mabasi Babati mkoani Manyara tarehe 12 Oktoba, 2023
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza akiangalia nakala ya gazeti la kwanza la Serikali baada ya Uhuru 1961 alipotembelea banda la Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Wiki ya Kimataifa ya kupunguza madhara ya maafa yanayoendelea katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mabasi Babati mkoani Manyara.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza akimsikiliza Mratibu wa UKIMWI kutoka TACAIDS Bw. Gilbert Mbwambo, wakati alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Wiki ya Kimataifa ya kupunguza madhara ya maafa yanayoendelea katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mabasi Babati mkoani Manyara.
Mratibu wa Maafa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bi. Numpe Mwambenja akitoa elimu ya masuala ya Menejimenti ya Maafa kwa wanafunzi wa Shule ya msingi ya Clare Ofassisi walipotembelea na kujifunza katika banda la ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Wiki ya Kimataifa ya kupunguza madhara ya maafa yanayoendelea katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mabasi Babati mkoani Manyara
Wanafunzi wa Shule ya msingi ya Clare Ofassisi wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) mara baada ya kutembelea na kujifunza masuala yanayoratibiwa na ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Wiki ya Kimataifa ya kupunguza madhara ya maafa yanayoendelea Babati mkoani Manyara.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa anayeshughulikia Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Prudence Constantine akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Singe walipotembelea banda la ofisi hiyo.
Mratibu wa Maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Salvatory Katamaza akitoa elimu kuhusu tahadhari ya mvua za El-nino kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Singe waliotembelea na kujifunza katika banda la ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho hayo.
…………………………..
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza ameiasa jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI nchini kwa kuendelea kuzingatia elimu inayotolewa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini ili kuunga mkono jitihada za Serikali dhidi ya mapambano hayo na kuyafikia malengo yaliyopo.
Ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu alipotembelea na kujionea shughuli zinazoratibiwa na ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Wiki ya Kimataifa ya kupunguza madhara ya maafa yanayoendelea katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mabasi Babati mkoani Manyara.Maonesho yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambapo yameambatana na uwepo wa maonesho mbalimbnali ya shughuli za uzalishaji, burudani, ujasiriamali na michezo iliyobeba jumbe za elimu kwa vijana katika kuipamba wiki hiyo.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa, jamii haina budi kuendelea kujilinda na kuwalinda wengine kwa kuzingatia ushauri na elimu inayotolewa ili kuhakikisha hali ya maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI nchini ipungua na kuyafikia malengo ya kuzifikia sifuri tatu ifikapo 2030.
“TACAIDS imeendelea kufanya kazi nzuri ya kuifikia jamii kwa njia ya elimu, ila endeleeni kuongeza nguvu kwa vijana kwani ndilo kundi linaloongoza kwa maambukizi bila kusahau ni kundi muhimu katika uzalishaji na kujiletea maendeleo yetu, hivyo elimisheni kwa nguvu watu wabadili mitazamo yao,” alisema Mhe. Hamza
Aliongezea kuwa, Tume iendelee kutoa elimu ya matumizi sahihi ya Kondomu ili kupunguza maambukizi ya VVU na UKIMWI hasa kwa kundi la vijana nchini.
“Endeleeni kufunga makasha ya kondomu katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo; kumbi za burudani, baa na nyumba za wageni lengo ni kuendelea kupunguza maambuki ya VVU na UKIMWI,” alisisitiza
Kwa upande wake Mratibu wa UKIMWI kutoka TACAIDS Bw. Gilbert Mbwambo akieleza majukumu ya Tume hiyo alisema kuwa Serikali imeboresha huduma za VVU na UKIMWI ikiwa ni pamoja na utoaji wa dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI kwa watu wenye maambukizi ya virusi hivyo pamoja na elimu ya matumizi sahihi ya Kondomu.