Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus akizungumza na kuwaelezea Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya Doha nchini Qatar na New Delhi India. Mkutano huo na Waandishi wa Habari umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Oktoba, 2023.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya New Delhi nchini India katika sekta ya Afya. Mkutano huo na Waandishi wa Habari umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Oktoba, 2023.
………………………..
Serikali imekubaliana na makampuni makubwa 2 duniani ya matrekta, Mahindra na John Deer kuweka katika kipindi cha miezi 12 viwanda vya kuunganisha matrekta na kutengeneza vipuri ndani ya Tanzania.
Hayo yameelezwa leo Ikulu jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus akiwa ameambatana na mawaziri wa kisekta na akizungumza na kuwaelezea Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliyofanya Doha nchini Qatar na New Delhi India.
Mkurugenzi huyo amesema katika ziara hiyo pia Tanzania imefanikiwa kupata uhakika wa soko la mbaazi na Rais Samia ameomba kupata allocation yaani kupatiwa soko la mgawo wa uhakika wa tani laki mbili kwa kuwa India ni mtumiaji mkubwa wa mbaazi duniani.
‘Pia katika ziara hiyo kulitiwa saini hati za makubaliano 15 zenye nia ya kuimarisha ushirikiano zaidi na India. Viongozi wa pande mbili walibadilishana hati hizo zikishuhudiwa na Rais Samia Pamoja na Waziri Mkuu wa India Modi. Hati 10 ni baina ya taasisi za serikali na hati 5 za sekta binafsi.’amesema Zuhura
Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akijibu swali la mwandishi wa habari amesema, katika mazungumzo na viongozi wa India, Tanzania imesisitiza umuhimu wa Wafamasia wa India kuzalisha dawa humu humu nchini ambapo hilo limefanikiwa na hatua hiyo italinufaisha soko la Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri Ummy amesema katika ziara hilo pia Hospitali ya Apollo ya India ambayo inamtandao wa hospitali 73 nchini India imekubali ombi la serikali kufungua tawi la Apollo nchini ili kusogeza huduma zao karibu na watanzania.
‘Tunataka kuifanya Tanzania kuifanya kuwa kitovu cha Tiba Utalii ili lengo letu ni katika maeneo ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kuhakikisha Tanzania tunakuwa na tiba za magonjwa mbalimbali’amesema Waziri Ummy
Aidha katika Sekta ya Kilimo,Waziri wa Kilimo Husein Bashe amesema Serikali ya Tanzania imewasilisha mahitaji kwenye serikali ya India kwa ajili ya mradi mkubwa wa umwagiliaji kutoka Ziwa Victoria ambapo Mahitaji hayo ni takriban dola Bilioni moja ambao mradi huo utatekelezwa mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida, Dodoma, Kagera na Mara.
‘Nimshukuru Mhe Rais kwani Mwaka mmoja uliopita wastani wa umwagiliaji tulikuwa tunatumia hekta laki saba na ishirini,mwaka huu miradi inayoendelea tutafika hekta Mill 1.2 na mwaka kesho tutaingiza kwenye bajeti hekta laki tatu hivyo mpaka 2025 tunataka kufika hekta Mill 5.;amesema Waziri Bashe
Naye Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema katika ziara hiyo Rais Samia ameonyesha nia ya kutaka kuyatoa maji Ziwa Victoria kupeleka Singida mpaka Dodoma ili kuwaondolea wananchi adha ya maji katika maeneo yao.
‘Ukiangali jiji la Dodoma kabla serikali haijaamia kwenye mji huu wakazi mahitaji yao ya maji ilikuwa ni Lita Mill 44,na Mamlaka yetu ya Maji ya DUWASA ilikuwa na uwezo wa kuzalisha maji Lita Mill 61 hivyo serikali ilivyohamia Dodoma kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu na hivyo kufanya mahitaji kuwa makubwa kufika zaidi ya Mill 140’amesema Waziri Aweso
Katika Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba,amezitaja sababu tano za ushirikiano na India kuwa ni pamoja na undugu wa muda mrefu,ushirikiano wa kidemokrasia kwa muda mrefu,uchumi wa India Teknolojia na Biashara lakini pia Bahari ya Hindi.
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya New Delhi nchini India katika sekta ya Kilimo. Mkutano huo na Waandishi wa Habari umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Oktoba, 2023.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya New Delhi nchini India katika sekta ya Maji. Mkutano huo na Waandishi wa Habari umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Oktoba, 2023.
Waandishi kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari nchini wakiwa kwenye Mkutano wa kuelezea kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya Doha nchini Qatar na New Delhi India. Mkutano huo na Waandishi wa Habari umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Oktoba, 2023.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa kuelezea kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya Doha nchini Qatar na New Delhi India. Mkutano huo na Waandishi wa Habari umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Oktoba, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza masuala mbalimbali kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya New Delhi nchini India. Mkutano huo na Waandishi wa Habari umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Oktoba, 2023.