Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amehawahakikishia Watanzania kuwa mradi wa maji wa miji 28 utakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa mwaka 2025.
Mhe. Aweso amesema hayo akiwa jijini New Delhi nchini India alipofanya mazungumzo na viongozi wa makampuni ya wakandarasi wanaotekeleza mradi huo .
Waziri Aweso ambaye yupo nchini India katika ziara ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya mazungumzo hayo akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof. Jamal Katundu na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini India Bwana Deo Dotto na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji Robert Sunday.
Akizungumza na Wakandarasi hao pamoja na Mkandarasi Mshauri na mwakilishi wa Benki ya Exim ya India ameeleza jinsi Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivyowezesha kukamilika kwa michakato ya Mradi huo kuanza baada ya kuchukua muda mrefu na kuhimiza kazi ifayike vizuri ikiwa ni kurejesha shukrani kwa kiongozi wa nchi na kutimiza ufanikishaji wa malengo yake ya “Kumtua Mama Ndoo Kichwan”i.
Ameahidi ushirikiano katika hatua zote katika kipindi cha utekelezaji wa mradi huo, Pamoja na hilo wadau wameshukuru uongozi wa Wizara ya Maji kwa kuridhia kukutana nao na kusikiliza changamoto zao na kutoa majibu.