Mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano na Uhusiano Kwa Umma DART William Gatambi akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotangaza kufungwa kwa kituo cha Kivukoni kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho leo Jumatatu Oktoba 9, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mohamed Kuganda-Meneja usimamizi wa mipango ya usafirishaji DART akifafanua jambo wakati wa mkutano huo kati ya Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka DART na Waandishi wa habari leo Jumatatu Oktoba 9, 2023 jijini Dar es Salaam.
Wakala wa mabasi yaendayo haraka DART Kwa kushirikiana na mamlaka ya dhibiti usafiri Ardhini LATRA wamesitisha matumizi ya kituo cha daladala Cha kivukoni ili kupisha upanuzi wa kituo Cha mabasi yaendayo haraka kivukoni, unaotarajiwa kuanza mwezi huu wa 10
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya DART Mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano na Uhusiano Kwa Umma DART William Gatambi amesema upanuzi wa kituo Cha mabasi yaendayo haraka kivukoni,Ujenzi unaotarajiwa kuanza mwezi huu wa 10
Amesema kuanzia tarehe 21 mwezi huu daladala hazitaruhusiwa kukitumika kituo hicho na badala yake daladala zilizokuwa zinatoa huduma kwenye kituo Cha Kivukoni zitatumia vituo mbadala vitatu ikiwemo pembezoni mwa Wizara ya Ardhi,PPF Tower na Posta ya zamani
Amesema kuwa waendesha bajaji wao wataendelea kufika eneo la Kivukoni kwa sababu wao hupaki bajaji zao kandokando ya barabara hivyo haziwezi kuathiri zoezi hilo la ujenzi.
Afisa Mfawidhi mamlaka ya Udhibiti wa usafiri Ardhini LATRA Mkoa wa Dar es salaam Rahim Kondo amewataka Wamiliki na watoa huduma kuzingatia ruti katika vituo mbadala vilivyoelekezwa kinyume chake watakumbana na mkono wa sheria hivyo ni muhimu wakazingatia tangazo ililotolewa ili kuepuka usumbufu watakaokumbana nao endapo watakaidi agizo hilo
Hatua ya Upanuzi wa kituo hicho Cha mabasi yaendayo haraka Cha kivukon mara kitakapokalimika kitakuwa nanuwezo wa kupokea mabasi hayo kutoka kwenye ruti za mbagala, Gongolamboto na Tegeta
Ifahamike kuwa kituo Cha mbadala pembeni mwa Wizara ya Ardhi kitahudumia daladala za Kigogo Sokoni,Buyuni Chanika,Machinga Complex na Tabata Chang’ombe Aidha kituo Cha PPF Tower kitahudumia daladala za Tegeta na Gongolamboto na kituo Cha posta ya zamani kitahudumia daladala za Kivule,Kisemvule,Tegeta,Kinyerezi na Mbande.