………………..
Adeladius Makwega-MWANZA
Wakristo wameambiwa kuwa mwanadamu amekuwa na changamoto nyingi, amekuwa na mahangaiko mengi, huku akivaa vazi linalobadilika badilika lakini Mwenyezi Mungu ameendelea kuwa na upendo mkubwa kwake , Mungu ameendelea kumuhurumia kila mara kwa kuwapeleka wajumbe wake, ili kumuelekeza namna inayompasa kuishi.
Hayo yamesemwa na Padri Samsoni Masanja, Paroko wa Parokia ya Malya katika misa ya kwanza ya Dominika ya 27 ya mwaka A wa Liturjia ay Kanisa, jumapili ya Oktoba 8, 2023 kati ka Kanisa la Bikira Maria-Malkia wa Wamisionari- Parokia ya Malya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza“Injili ya leo (Mt ,21:33-43) inatukumbusa kuwa taifa teule lilifanya kosa wakati huo na hata sisi tunaweza tukayafanya makosa yale yale, hivyo huyu mwenye nyumba ni Mungu, shamba la mizabibu ni habari za ufalme wa Mungu na huo mzabibu ni taifa la Mungu ambalo Mungu mwenyewe analiweka hapo ambalo ni taifa teule , anapotuma wafanyakazi ni hao ni watenda kazi lakini matokeo yao wanawafanyia mabaya na mwisho anampeleka mwanae nayeye wanamkamata na kumuua .
Hapo ndipo mwenye shamba atawaangamiza wote na kuweka wakulima wengine.”Padri Masanja alimalizia mahubiri haya akisema kuwa Wakristo wana bahati kubwa ambayo awali haikuwa yao, hivyo waitumie bahati hiyo vizuri na hawatakiwi kufanya kosa walilofanya taifa la Israel.
Mara baada ya mahubiri hayo sala ya Nasadiki ilisaliwa na ulifika wakati ya nia na maombi ya misa hii ya dominika.
“Eee Baba Mungu utupe bidii ya kufanya kazi kwa bidii katika shamba lako, yaani Kanisa na kuzaa matunda mema katika shamba lako , ee Bwana, twakuomba utisikie.”
Hadi misa hiyo ya kwanza iliyoanza saa 12. 00 inamalizika, hali ya hewa ya Malya na viunga vyake kwa juma zima ilipata mvua kwa siku moja tu, huku baadhi ya wakulima wakisubiri mvua kubwa kunyesha ili kupitisha majembe ya kukotwa na wanyama kazi na matrekta mashambani, wakulima wachache waliopanda mapema mahindi yao mashamba yakiendea vizuri.