NA NOEL RUKANUGA

Wekundu wa Msimbazi Simba Sc wamefanikiwa kuibuka na ushindi ugenini wa mabao mawili kwa moja dhidi ya  Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa leo Oktoba 8, 2023 katika Uwanja wa Liti  Mkoani Singida.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Liti umesoma Singida Big Stars 1-2 Simba.

Bao la Saido Ntibanzokoza dakika ya 26 lilikuwa la mipango na bao la pili la Moses Phiri lilikuwa ni pigo kubwa kwa Singida Big Stars baada mpira kumshinda Beno Kakolanya.

Bao la Singida Big Stars  lilifungwa na Deus Kaseke kutokana na makosa ya Ally Salim katika kuokoa hatari.

Simba Sc inaongoza Ligi ikiwa na Pointi 15 ikiwa  baada ya kucheza mechi tano msimu wa 2023/24.

Bingwa mtetezi Yanga  naye alipata matokeo ugenini  katika mchezo uliopita baada ya kushinda  mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold.