Na Sophia Kingimali.
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Mhimbili (MOI) imesema itaendelea kuwa wabunifu katika huduma kwa kufanya na kuendeleza utalii kupitia sekta ya Afya(afya utalii) kwa kuweka huduma mpya na kuhakikisha huduma zao zinaendana au zaidi na huduma zitolewazo nje ya nchi.
Akizungumza leo Oktoba 8 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu, Dk. Laurent Mchome alipotembelea onesho la saba Site Swahili Internation Tourism Expo yanayoendelea jijini Dar es salaam amesema wao wanaonesha huduma zao ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kupanua tiba na huduma zao ndani ya nchi na nje lakini kuboresha sekta ya utalii kupitia afya.
Amesema kuendana na sera ya Tiba Utalii MOI walifungua tawi la huduma hiyo kwaajili ya wagonjwa wa nje ya nchi na watanzania wanataka kutumia huduma hiyo.
“MOI wana tuna huduma nyingi za kibobevu ikiwemo za vifaa bandia ikiwemo mikono na miguu bandia kwa sasa hivi tuna mikono bandia ambayo ni smart unaweza kufanyia kazi mkono wa bandia kunyanyua maji kushika karamu,gazeti yote hii ni kuhakikisha tunatatua huduma na kujiweja katika ngazi ya kimataifa,” amesema Dk. Mchome.
Amesema ya upasuaji wa ubongo, mgongo, mifupa pamoja na viungo hivi wamekuwa wakifanya kwa mda mrefu kwani ndio kituo kuu kwa Afrika Mashariki na Kati.
Amesema wameendeleza huduma hizo kwa kiwango kikubwa sasa hivi wanafanya huduma ambazo hawapasui kwa kiwango kikubwa kama zamani sasa wanapasua kwa kiwango kidogo kwa njia ya matundu.
Ameeleza kuwa upasuaji huo wanafanya kwenye magoti, nyonga kiwiko cha mikono na kwenye mabega ambao umeanza siku za hivi karibuni.
“Tunahakikisha kwamba sehemu ambazo tunafanya upasuaji zinakuwa ndogo ili kuepusha makovu makubwa kwenye mwili”amesema.
Aidha amesema wanafanya upasuaji wa surgery kwenye mgongo kwa matundu madogo kuacha upasuaji mkubwa ambao unakaa siku nyingi.
Amesema upasuaji wa matunda ukinafanyika unasaidia kukaa mda mchache hospitali na kuruhusiwa mapema.
Dk. Mchome ameongeza kuwa wanafanya upasuaji wa kutoa uvimbe chini ya uvungu wa ubongo kwa kutumia njia ya kupitia puani.
“kwenye ubongo kukiwa na uvimbe Mara nyingi unatakiwa kutolewa kupitia juu lazima ufungue fuvu lakini hii ni tofauti kwani unaweza kutolewa kupitia kwenye pua bila kufungua fuvu”amesema.
Amesema hadi sasa ni miaka mitano tangu kuanza huduma hiyo na wana wataalamu wa bobezi katika huduma hiyo.