Waziri wa uchukuzi Prof.Makame Mbarawa akikagua tuta la reli ya kisasa akiwa na viongozi wa mbalimbali wa shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na mkandarasi Yapi Merkezi.
Mitambo ya Mkandarasi Kampuni ya Yapi Merikezi ikiwa kazini .
Waziri wa uchukuzi Prof.Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa mkanadari wa reli ya kiksasa kulia na kushoto ni Kaimu mkurungezi mkuu wa TRC ,Mhandisi Senzige Kisenge aliyevaa shati la Bluu
……
Na Lucas Raphael,Tabora
Serikali imesema bado hajiridhishwa na kasi ya ujenzi wa reli ya kisasa SGR kipande cha Makutupora – Tabora huku akimwagiza mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi huo ili kuendana na muda elekezi wa kimkataba.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa uchukuzi Prof.Makame Mbarawa alipokuwa katika ziara mkoani Tabora alipokuwa anakagua mradi huo wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Makutupora – Tabora chenye urefu wa kilometa 368 ambapo amesema ujenzi huo kwa sasa ulikuwa unatakiwa kuwa umefikia asilimia 22 ukilinganisha na sasa upo asilimia 12.
Alisema kwamba kufuatia kusua sua kwa kasi ya ujenzi wa mradi huo amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kupitia kampuni ya kigeni ya Yapi Merkezi kuongeza kasi ya ujenzi ili kufidia muda wa asilimia 10 ambao umepotea katika utekelezaji wa mradi huo.
Hata hivyo alitoa agizo kwa shirika la reli Tanzania (TRC) kuhakikisha wanaendelea kusimamia viwango vya ubora katika mradi huo.
Prof. Alisema viongozi wanaosimamia wakijipanga vizuri na kuweka mikakati yao itasaidia kurudisha mpango wao wa kumaliza kwa wakati ujenzi huo.
Waziri huyo alisema kwamba bado anaamini kuwa viongozi watasimamia vizuri na mradi utamalizika na changamoto zitakwisha na watasonga mbele.
“Changamoto katika ujenzi wa tuta kuna mambo ya msingi nitazungumza na Mkandarasi Yapi Merikezi kuhakikisha mradi unakwenda haraka na watafanyakazi ili ule muda uliopotea utakaa vizuri” alisema
Aliwapongeza TRC kwa kumpa fulsa ya kutembelea mradi huo wa reli ya kisasa SGR kutoka Makutupora hadi Tabora.
Naye Kaimu mkurungezi mkuu wa TRC ,Mhandisi Senzige Kisenge amekiri kuwepo kwa changamoto ya kutoteleza mradi huo kwa wakati kwa sababu ulianza mwezi Machi 8 mwaka 2022 na mkataba kumalizika januari 2026.
Alisema kipande cha kwanza Dar-es -salaam hadi Morogoro kilometa 300, imefikia asilimia 98.5 na cha pili Morogoro – Makutupora kilometa 422 kimefikia asilimia 94 ,Makutupora -Tabota 368 upo asilimia 12.
Kwa upande wake Meneja Mradi huo,Mhandisi Edwen Ntahondi alisema ujenziwa SGR kipande cha tatu una jumla ya kilometa 294 kwa njia kuu na kilometa 74 njia za kupishana.
Alisema kwamba Mkataba wa utekelezaji huo ulianza 8 marchi 2022 na muda wa utekelezaji ni miezi 42 na unatarajiwa kukamilika mnamo januari 2026.
Alisema kwamba Hadi kufika septemba 2023 maendeleo ya mradi yalikuwa asilimia 12 ikilinganishwa na mpango kazi wa asilimia 22,hivyo mradi ulikuwa nyuma kwa asilimia 10 na Mkandarasi ameelekezwa kufanya mapitio ya mpango kazi wake na kuandaa upya ili kufidia muda uliopotea.
Ujenzi wa reli ya kisasa maarufu kama SGR kipande cha Makutupora – Tabora unatekelezwa kwa gharama ya zaidi shilingi Trioni 4.